CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Wednesday, February 19, 2014

MZEE KIFICHO ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA MUDA WA BUNGE LA KATIBA

Mhe. Pandu Ameir Kificho
(Spika wa Bunge la Wawakilishi - Zanzibar, na
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba)
Mhe. Pandu Ameir Kificho (Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar) amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba katika uchaguzi uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

Mhe. Kificho aliibuka na ushindi wa kura 393 kati ya kura 558 zilizopigwa, sawasawa na 69.19%. Washindani wengine walikuwa ni Mhe. Magdalena Rwebangira na Mhe. Costa Mahalu, ambao kila mmoja alilipata kura 84, sawasawa na 15.79%.

Aidha akitangaza matokeo hayo, Katibu wa Bunge Dkt.Thomas Kashilila alisema kuwa mgombea wa nne, Mhe. Sadifa (ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM na Mbunge kutoka Zanzibar), aliamua kujitoa katika hatua za mwisho za kujinadi kwa wajumbe. Mhe. Sadifa alisema kaamua kujitoa kwa kuwa anamheshimu Mhe. Kificho na hivyo aliona ni vyema akamuachia.

Kwa mujibu wa sheria, Mwenyekiti wa Bunge la Katiba ndiye atakuwa na mamlaka ya kusimamia zoezi la Kutunga Kanuni zitakazotumika kwenye Bunge la Katiba.

No comments: