CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Sunday, November 28, 2010

Tawi la CCM Moscow Lafanya Sherehe Kumpongeza JK

Na Mwandishi wetu Happy    
        Katika hali iliyoonekana kuwavutia watanzania wengi waishio nchini Urusi, Tawi la CCM Moscow limefanya sherehe ya kumpongeza Mwenyekiti wa CCM na Raisiwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni. Sherehe hiyo iliyoanza majira ya saa kumi na moja jioni ya tarehe 27/11 na kumalizika majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi ya tarehe 28/11 iliwavutia sii tuu watanzania waishio nchini Urusi na Maeneo ya jirani, bali pia natu wengine wasio watanzania.
       Miongoni mwa wageni muhimu waalikwa na Capt. Mstaafu Jaka Mwambi ambaye pia aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi Tanzania ikiwemo ukatibu mkuu msaidizi wa CCM Taifa. Mh. Mwambi katika htuba yake kwa wapenzi, wanachama na wakereketwa wa CCM waliohudhuria amesisitiza kuwa vijana sio tuu taifa la kesho, ila pia ni Taifa la Leo na la Keshokutwa. Mh. Mwambi amesema kuwa vijana wasifikirie kuwa kujiunga na chama ni kujinufaisha kifedha, bali ni kukomaa kimawazo na kisiasa na lengo kubwa ni baadae kuwatumikia wananchi na sio wananchi kuwatumikia.
     Mwenyekiti wa Tawi la CCM Urusi Dk. Alifred Kamuzora katika hotuba yake alihoji kuwa katika uchaguzi wa hivi karibuni, ambapo wapinzani wanadai matokeo yalichakachuliwa, isije kuwa wenyewe wanaotoa madai hayo ndio waliojichakachua wenyewe. Akisisitiza jambo, Dk. Kamuzora alisema Matokeo ya Uchaguzi kuanzia ya uraisi hadi wabunge na madiwani yalikuwa sio ya ubabaishaji na uchaguzi ulikuwa huru na, salama na Haki, hata taarifa ya waangalizi wa Umoja wa Ulaya, Umoja wa Africana SADC walithibitisha hilo. Aither Dr. Kamuzora alisisitiza kuwa katika kipindi cha mwanzo cha uongozi wa Raisi Kiwete CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutimiza ilani yake ya uchaguzi. Katika kauli mbiu ya CCM ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania, CCM imeweza kuboresha huduma za hospitali, kuongeza  shule za msingi, shule za sekondari kwa kila Kata na hata vyuo vikuu nchini vimeongezeka kutokana na sera na Ilani ya CCM.  Mengine ni uboreshaji wa mahakama huru, ambapo watanzania wameshuhudia hata watu waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini wakisimama kizimbani, uboreshwaji wa chombo imara cha dola, jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi, na Jeshi la kujenga Taifa.
     Aidha, CCM imeweza kuboresha elimu, maji, umeme, barabara nk. hayo ndio maisha bora yanayozungumzwa.
Kutoka Kushoto ni Katibu wa Uchumi, Mipango na Fedah wa Tawi Ndg. Boniface Assenga anayefuatia ni Mwenyekiti wa Tawi Dk. Alfred Kamuzora akifuatiwa na Katibu Mkuu wa TAwi Bi. Neema Kengese na anayefuatia ni Ndg. Salim Mfungahema Katibu wa Siana, Sera na Uenezi wa Tawi

No comments: