CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Wednesday, April 14, 2010

MAELEZO MAFUPI YA MW/KITI WA UVCCM -URUSI JUU YA UWASILISHAJI HOJA ZA BARAZA LA VIJANA TAWI


UVCCM CHAIRMAN REMARKS: MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA TAWI CCM-MOSCOW 13/12/2009:
UWASILISHAJI WA HOJA :-MAAZIMIO YA BARAZA KUU LA VIJANA 2010-2011 NA TAARIFA YA ZIARA YA KIUTENDAJI-TANZANIA:
Mheshimiwa mwenyekiti wa tawi la CCM-MOSCOW:
Waheshimiwa wajumbe wa secretarieti , kamati ya siasa ya tawi
Waheshimiwa wajumbe wateule toka jumuiya ya vijana.:


Kama ilivyo ada yetu ,tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa afya na uzima hadi tukakutana tena leo katika kikao muhimu ndani ya tawi letu, kitakachotoa dira na muelekeo wa kimaendeleo hapa Urusi.
Kwa namna moja niseme …., Pongezi kwa Wana ccm wote, Kutokana na Matokeo ya Uchaguzi wa serikali za mitaa huko Tanzania Bara. CCM ni chama bora na kinakubalika na watanzania wa rika zote.. Katika Uchaguzi wa serikali za mitaa oct 2009 , CCM ilishinda kwa 90%, . Mafanikio haya ni makubwa na yanahitaji kupongezwa. Hatuna budi kukubali kuwa CCM ni Chama imara na madhubuti kutokana na Takwimu za uchaguzi wa serikali za Mitaa.
Ndugu wajumbe , ningependa kutoa rai kw awanachama wote kuwapuuza wale wote ambao hawaitakii mema CCM, kauli mbalimbali za wanaasisa/mashirika yasio ya kiserekali nk, zisiwe chanzo cha kusambaratisha umoja wetu bali ziwe ni kichocheo cha Uwajibikaji kisera na kifikra endelevu kutokana na mabadiliko ya Kimfumo na yenye tija kwa wanachanchi wote. Wana CCM hatuna hasa Vijana ,hatuna budi kuanza harakati mpya za mabadiliko ya kimfumo endelevu ndani ya chama kutokana na mabadiliko ya siasa za dunia.
Ndugu wajumbe ,Binafsi naamini serikali inayongozwa na CCM ina vikao husika na mihimili ya dora husika katika kutoa ufumbuzi yakinifu wa hoja zinazojengwa na wanasiasa /wananchi kwa maslahi ya nchi. Naamini wale wote waliohusika katika matumizi mabaya ya madaraka yao,baada ya uchunguzi kukamilika watafikishwa katika vyombo vya sheria ili kujibu tuhuma zinazowakabili, kama ambavyo utekelezaji wake unaendelea sasa.
Naomba ninuku, baadhi maneno ya mwenyekiti CCM alisema ……..“ Lazima tuendelee kuzihusisha sera zetu na wakati. Chama chetu hakina sera zilizoganda bali ni nyumbufu zinazotambua mabadiliko ya nyakati na kwenda nayo sambamba, zaidi ya hayo, chama chetu kina sifa ya kutekeleza sera zake na ahadi zake kwa wananchi kwa mafanikio makubwa. Kimefanikiwa kufanya hivyo kwa sababu ya kushika hatamu za uongozi na kuzisimamia vyema serikali zake….
Kwa upande mwingine Mhe. Mwenyekiti CCM na Raisi wa Tanzania aliwakumbusha viongozi na watendaji wa chama mahali popote juu ya dhana ya uwepo wao katika chama , alisema
chama imara ni kile ambacho viungo vyake vimekamilika na vinafanya kazi vizuri .chama ni wanachama ,viongozi,vikao ,watendaji ,rasilimali na jumuiya za chama “.

Ndugu wajumbe ‘ tambueni kuwa tunaweza kujenga tawi letu kuwa imara na endelevu .kukidumisha na kukiendeleza chama chetu ili kiendelee kuwa tumaini na kimbilio la watanzania wote waishio Urusi na maeneo ya jirani ,Yote haya yanawezekana ikiwa tu utatimiza wajibu wetu kwa jukumu ulilopewa kama mwana CCM na chipukizi.
Ni muhimu tujenge uelewa wa kutambua taratibu na miongozo ya chama chetu, ni muhimu tuwe na wakati binafsi kusoma miongozo yote ya chama, au taarifa za kichama kwa kusoma kupitia internet au vitabu vya kiada na ziada. Kwa kufanya hivyo , tutakuwa na uelewa wa chama na sera zake, na pia utakuwa madhubuti katika kukitangaza chama na kamwe hautaweza kuyumbishwa na mtu yeyote.
Udhaifu wa kutoelewa miongozo na taarifa hizi ni hatari sana kwa maendeleo yako mwenyewe katika utendaji wa serikali /chama na pia hupelekea kudidimiza maendeleo ya tawi

Ndugu wajumbe Takwimu za mkutano wa awali, unaonyesha kuwa baadhi ya wajumbe walioteuliwa kuwa wajumbe wa halmashauri kuu, walikubali uteuzi huu, Nawashukuru wajumbe wote waliokubali uteuzi huu, lakini wajumbe kadhaa, hawakuweza kutii tamko la kuhudhuria baadhi ya vikao husika. Mpaka sasa hakuna taarifa zozote za kimaandishi zilizowasilishwa kwa kwa mwenyekiti wa tawi kuhusu sababu za kutohudhuria kwao katika tarehe husika. Tuache udhaifu katika hili. Udhaifu huu ni jambo lisilofurahisha hata kidogo na hatuna budi tubadilike !
Ndugu wajumbe !Mtambue kuwa tofauti na mfumo wa serikali, katika CCM maamuzi hufanywa kupitia vikao kwani, kutofanyika kwa vikao vya chama vya ngazi husika kunadhoofisha sana mfumo mzima wa maamuzi ndani chama (kitawi) na kunaua dhana nzima ya demokrasia ya ndani ya chama na dhana ya uongozi wa pamoja.
Ni vema kuwa na utaratibu ; Taarifa za kimaandishi za kutohudhuria kikao husika, ziwasilishwe siku mbili kwa katibu wa Tawi .ili sasa kutokana na ratiba ya vikao vya halmashauri /kamati ya siasa ya tawi hili kwa mwaka 2009/10, idadi ya vikao na tarehe husika ijulikane. Endapo mjumbe hataudhuria viakao 2 na zaidi bila taarifa rasmi ni vema sasa halmashauri hii ,ipitishe utaratibu mbadala kwa mjumbe husika, kutoa maamuzi ya msingi.
Ndugu wajumbe :Nawasihi mpitie na mtafakari taarifa ya utekelezaji wa ziara yangu, ili kufahamu kichojiri katika ziara hiyo na uelewa wa taarifa kwa husika. Ambatanisho na hilo ni pamoja na Taarifa ya Maazimio ya Baraza kuu la vijana lilokutana tarehe 06/12/2009.
Baada ya kutafakari kwa makini riport hii ya Ufanisi wa ziara kichama na maazimio ya baraza , ningependa kueleza japo kwa ufupi mradi wa kuimarisha tawi letu hapa urusi , kama ilivyoanishwa kimalengo katika mkutano wa kamati ya siasa ya tawi ilifanyika june 2009.
Ndugu wajumbe , Nafikili:-wakati ni huu kuendelea kutoa msukumo maalumu wa kuhakikisha kuwa madhumuni ya miradi na mikakati tuliojiwekea yanafanikiwa hususani maazimio 14 ya baraza kuu la vijana tawi
Kubwa zaidi katika kutekeleza miradi na maazimio haya ni kuhakikisha kwamba wanachama wa CCM katika tawi wanaongezeka . Wanachama ambao ni Imara kukitetea na kulinda chama chao.Wanaolipa ADA zao kwa wakati na kuchangia maendeleo ya chama chao
Pili kuhakikisha kuwa chama chetu kinatoa viongozi walio madhubuti, yaani waaminifu kwa chama, waadilifu,wachapakazi hodari na jasiri kukipigania chama chao.
Tatu , ni lazima tuendelee kusimamia maadili ya mwanachama ,viongozi na uongozi/mtanzania ndani na nje ya chama .
Mwisho, naamini tukiyatelelza haya, kwa ukamilifu katika muda huu muafaka wa mabadiliko, tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika kuimarisha tawi letu na kuzidisha imani kwa wanachama wa CCM na watanzania wote waishio Urusi na maeneo ya Jirani
Naomba mkutano huu wa halmashauri kuu Kuridhia Maazimio ya Baraza la vijana , itakayotoa dira na muelekeo wa shuguri za tawi na wanachama wote kwa mwaka 2010/2011.

Baada ya kuzungumza hayo machache, Mheshimiwa mwenyekiti naomba kuwasilisha TAARIFA YA UTEKELEZAJI KUHUSU ZIARA YA MW/KITI WA UVCCM –URUSI , DAR ES SALAAM TANZANIA ( 17-21 /8 /2009). NA TAARIFA YA MAAZIMIO 14 YA BARAZA KUU LA VIJANA LA TAREHE -6/12/2009 kwa mwaka 2010-2011.

Mheshimiwa mwenyekiti , Naomba kuwasilisha!!!
Chrispin Bakunda 13/12/2009
Mwenyekiti Jumuiya Vijana- CCM-MOSCOW.

No comments: