CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Saturday, April 17, 2010


Rais Kikwete ayapokea maandamano ya UVCCM ya kumuenzi marehemu Mzee Abeid Karume Zanzibar


Rais Jakaya mrisho Kikwete, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar(kulia) na Mwenyekiti wa jumuiya ya umojawa Vijana wa CCM Bwana Yusuf Masauni wakati wa mapokezi ya maandamano ya umoja wa vijana wa CCM mjini Zanzibar jana jioni.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa Vijana CCM Yusuf Masauni(wapili kushoto), Makamu mwenyekiti wa jumuiya hiyo Bwana Beno Malisa(kushoto), na katibu mkuu wa jumuiya ya umoja wa Vijana CCM Bwana Martin Shigela wakiyapokea maandamano ya vijana wa CCM katika viwanja vya CCM Maisara Zanzibar jana jioni.Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyekuwa mgeni Rasmi katika maandamano hayo aliwahutubia vijana hao.
Baadhi ya vijana wananchama wa UVCCM wakishangilia hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa wakati wa kilele cha maandamano yaliyoandaliwa na jumuiya hiyo mjini Zanzibar kumuenzi muasisi wa mapinduzi ya zanzibar marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Mjane wa Muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar Mama Fatma Karume pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Shadya Karume wakati wa dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyosomwa wakati wa kilele cha maandamano ya UVCCM kumuenzi muasisi huyo jana mjini Zanzibar.
Msimaji
Zanzibar

No comments: