CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Wednesday, April 14, 2010

TAARIFA KWA WANACHAMA KUHUSU MCHAKATO WA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAWI



 TAARIFA KWA WANACHAMA: 

Halmashauri  Kuu ya Tawi la CCM moscow ,  imefanya mkutano wa kawaida tarehe  27 March, 2010 chini ya Katibu Kiongozi, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tawi  Ndugu Alfredi Kamuzora mjini Moscow.

Katika mkutano huo Halamsahauri Kuu ya Tawi imejadili masuala mbali mbali kuhusu hali ya kisiasa katika Tawi, maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Viongozi wa Tawi, kuanzia ngazi za mashina, Jumuia za ccm tawi, pendekezo la jina la katibu wa tawi iliokuwa wazi baada ya Bwana  Swilla L.M. kuomba kupumzika, kutokana na majukumu yake binafsi kuongezeka  ambapo  aliwasilisha barua ya kujiuzuru kwanye  kamati ya siasa, na kamati ya siasa iliridhia ombi lake.

Halmashauri kuu ya Tawi , imemteua  Bi NEEMA CHARLES KENGESE , kuwa katibu wa tawi  mpya, ili kuziba pengo lilikuwa wazi kutokana na kujiuzuru kwa Bwana Swila L.M. 
Pia,halmashauri kuu ya tawi, inazidi kuwasisitiza wanachama kushiriki kikamilifu katika zoezi la ukusanyaji  PICHA moja na rub 50 ikiwa ada ya uachama na kuchangia gharama za uandaaji wa Tafrija ya UGAWAJI WA KADI ZA UVCCM ambapo imepangwa kufanyika MAY 2010, 
KUHUSU MCHAKATO WA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAWI:  Halimashauri kuu ya tawi , imejadili kwa kina:kifungu kwa kifungu MWONGOZO WA UCHAGUZI WA TAWI, ambapo :- Mchakato wa Uchaguzi wa Viongozi wa CCM tawi la ccm moscow utaanza kutekelezwa Mwezi February, 2011 kwa uchaguzi wa viongozi wa mashina,wajumbe wa halmashauri kuu ya tawi.Tarehe 10 May 2011 ni uchaguzi wa mwenyekiti wa Tawi ikifuataiwa na kuapishwa kwa uongozi mpya wa Tawi la CCM  moscow .
Uchaguzi huu ni wa kawaida na nafasi za kugombea zitazingatia  katiba ya CCM ,Kanuni ya UVCCM na Mwongozo wa tawi. Ratiba ya Uchaguzi imeambatanishwa na Taarifa hii.Pia unaweza kusoma na kuelwa zaidi Maelekezo kuhusu Mchakato wa Uchaguzi wa Viongoz wa tawi kwa kubofya "habari za uchaguzi " kwenye ukurasa wa mbele wa Tovuti tii 
au bofya hapa

Maelekezo kuhusu Uchaguzi yanatolewa kwa Madhumuni ya kutoa Taratibu zitakazowezesha kufanyika maandalizi mazuri yatakayofanikisha Uchaguzi huo. 
Kwa madhumuni ya kufanikisha uchaguzi , Msimamizi wa uchaguzi (kamati ya siasa) itateteua waandamizi 2 chini ya Katibu wa Tawi(mkurugenzi wa uchaguzi) ambao wataandikisha na kuandaa  orodha ya wapiga kura (wanachama wa ccm wenye sifa) katika kila shina.  Ratiba imeambatanishwa:-


No comments: