CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Tuesday, May 4, 2010

Mkutano mkuu wa CCM Tawi la Moscow

CHAMA CHA MAPINDUZI.
TAWI LA MOSCOW –URUSI.
02 May 2010.


TAARIFA KWA WANACHAMA, WAPENZI NA WAKEREKETWA CCM-TAWI LA MOSCOW-URUSI JUU YA KUITISHWA KWA MKUTANNO MKUU WA TAWI.
Husika na kichwa cha habari hapo juu, napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu ya kuwa barua yenu niliyoipokea tarehe 25 april 2010 kuhusu ombi la kuitishwa kwa mkutano mkuu wa Tawi CCM –Moscow imeshughulikiwa , pia naomba radhi kwa kutofanikisha mkutano huo tarehe 02 may 2010 kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu.. Kwa mujibu wa katiba ili kuitishwa kwa mkutano mkuu ni lazima Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya Tawi ijadili agenda na kupanga tarehe ya mkutano na baada ya hapo kuitisha mkutano wa Halmashauri kuu ya Tawi ili iweze kupitisha agenda hizo.
Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya Tawi ilifanya kikao chake tarehe 02 may 2010 na ilikubaliana kuwa itaitisha kikao cha Halmashauri Kuu ya Tawi tarehe 09 may 2010 na tarehe 23 may 2010 ndio tarehe iliyopangwa kwa ajili ya mkutano mkuu wa CCM- Tawi la Moscow Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Tawi ilipenda sana mkutano huo ufanyike tarehe 16 may 2010 lakini haitawezekana kwa sababu siku hiyo itakuwa ni siku ya uchaguzi mkuu wa viongozi wa jumuiya ya wanafunzi wanaosoma chuo cha Lumumba (TSU). Mahali na muda kamili wa mkutano huo mtajulishwa mara tu baada ya mkutano wa Halmashauri Kuu ya Tawi.


KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.


Katibu wa Tawi
CCM-Moscow
Bi. Kengese Neema C.

No comments: