CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Wednesday, September 29, 2010

Waziri wa Elimu Tanzania Visiwani Haroun Ali Suleiman, naibu Waziri wa Elimu Mh. Gaudensia Mugosi Kabaka watua Moscow

Moscow-Russia 29.09.2010 22:46.47
Na Mwandishi wetu

Waziri wa Elimu Tanzania Visiwani Mh. Haroun Ali Suleiman, naibu Waziri wa Elimu Mh. Gaudensia Mugosi Kabaka wapo mjini Moscow - Urusi kuhudhuria mkutano wa Kimataifa. Pamoja na Watumishi wengine waandamizi wa serikali ya Tanzania, Waziri Suleiman ameongozana pia na Makatibu wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana.

Mara baada ya kujumuika na wenyeji wao kwa chakula cha Jioni Katika Ubalozi wa Tanzania uliopo hapa Moscow, Waziri Suleiman alisema kuwa Zanzibar kwa sasa ni tulivu na utulivu huu ambao haujawahi kutokea hasa katika kipindi cha uchaguzi kama hizi, unatokana na Juhudi za Rais Karume na jitihada za mpinzani wake Maalim Seif kusaini makubaliano ya kudumisha utulivu na kufikia muafaka kwa kuunda serikali ya mseto visiwani humo. Akitoa wito kwa wanafunzi wanaosoma nje ya nchi, waziri Suleiman ameshauri vijana kurudi nyumbani mara moja baada ya kuitimu masomo yao na kuwatoa wasiwasi wahitimu kuwa ajira ni nyingi sana na zimekosa wataalam. Akizungumzia kuhusu habari zake mwenye za kisiasa, ikikumbukwa kuwa Waziri Suleiman i mmoja wa waliojitokeza kuwania kiti cha uraisi visiwani Zanziba alisema kuwa Dr. Shein Aliponea chupuchupu kwa kuwa yeye alikuwa moto wa kuotea mbali na mwiba mkubwa katika king'ang'anyiro hicho. Waziri Suleiman hakusita kumwaga sifa zake kwa Balozi wa Tanzania Hapa Moscow Mh. Jaka Mwambi kwa mapokezi mazuri na kwa chakula safi cha jioni

Naye Balozi wa Tanzania Mh. Jaka Mwambi akiwa ndiye mwenyeji wa Msafara huo alipopata wasaa wa kupokea shukrani lukuki toka kwa ujumbe huo, aliiasa serikali ya Tanzania hasa wizara Mbalimbali kuutumia ubalozi wao wa Tanzania uliopo hapa Moscow kwa Ukaribu zaidi. Pia Mh. Balozi hakusita kueleza malalamiko ya wanafunzi wanaosoma nchini Urusi kwa namna ya kipekee kwa Mh. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Mh. Gaudensia Kabaka kuwa maisha ya hapa Moscow yamekweda juu kabisa kuliko mji mwingine wowote hapa duniani baada ya ule wa Japani - Tokyo

Naye Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Mh. Gaudensia Kabaka (anayefahamika hapa Moscow Mama Kabaka) aliahidi kufikisha malalamiko yote ya wanafunzi kwenye dawati husika na kuahidi kuwa wanafunzi sasa wakae mkao wa kula. Akizungumza na The THOMCOM, Mama kabaka alisema kuwa yeye Kama Mama, hapendi kuona wanafunzi wanalala nje kwenye baridi wakidai jambo la msingi ambalo linawezekana kabisa kutatuliwa. 
Mama Kabaka ambaye ni Kipenzi cha wanafunzi wengi hasa wanaosoma Moscow na nje ya nchi aliahidi kuhakikisha masuala yote yanayohusu wanafunzi na hasa posho zao yanaangaliwa tena ili kuhakikisha kuwa wanapata posho inayoendana na hali halisi ya mahali husika. Ikumbukwe kuwa Mh. Naibu Waziri Gaudensia Kabaka alishawahi kufika Moscow mwaka 2007 na kukutana na Wanafunzi wa kitanzania hapa Urusi na kuahidi ongezeko la posho na ahadi hiyo ikatekelezwa mwaka uliofuata kwa ongezeko la zaidi ya asilimia 68 na mwaka uliofuata ongezeko likafikia karibu asilimia 62.

 Picha

No comments: