CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Wednesday, November 10, 2010

BARUA YA PONGEZI KWA RAISI MTEULE WA JAMHURI YA MUUNGAN WA TANZANIA TOKA TAWI LA CCM MOSCOWYAH: PONGEZI KWA RAIS MTEULE DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE
Mh. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, uongozi wa Tawi la CCM Moscow pamoja na wanachama wake wote unapenda kuchukua nafasi hii ya pekee, kwa heshima na taadhima kukupongeza wewe ukiwa Raisi mteule na mwenyekiti wa Chama tawala cha CCM kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kuliongoza taifa letu la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Ushindi mkubwa ulioupata unadhihirisha kazi nzuri uliyoifanya katika kipindi kigumu cha miaka mitano, ni dhairi kwamba kauli mbiu ya chama imetekelezwa kwa kiasi kikubwa, hii imeongeza imani kwa watanzania. Ni kwa sababu ya sifa na uwezo ulionao uliweza kwa kipindi chote cha awamu ya kwanza ya uongozi wako ukiwa madarakani umeweza kuliwakilisha taifa letu kikamilifu katika nchi za nje hii imezidi kuliletea Taifa letu na watu wake sifa ya pekee.
Mh. Rais, naomba nikupongeze kwa kazi ngumu na ya muhumu uliyoifanya ya kulinda na kutetea hitoria ya amani ya nchi yetu, hii imetotana na uwezo wa upeo wako mkubwa ambao umeweza kukiongoza chama ukiwa kama Mwenyekiti wa chama Tawala na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kudumisha muungano kwa kuondoa machafuko ya kisiasa nchini, kama si uwezo wako na viongozi wa ngazi za juu wa Chama na Serikali uliokuwa nao sambamba katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo zito, nchi yetu ambayo ni kinara cha amani katika bara zima la Afrika ingepoteza sifa hiyo ya kihistori katika bara letu la Afrika.
Mh. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikweta kupitia kwako Tawi la Moscow lingependa kuchukua nafasi hii kuupongeza uongozi mzima wa CCM Taifa ambao bila shaka ulishilikiana katika mchakato mzima wa kampeni za uchaguzi kwa kutangaza kauli mbiu ya Chama Cha Mapinduzina na utekelezaji wake, hii imechangia kuleta ushindi mkubwa kwa Chama chetu cha CCM. Ni kweli kabisa katika ushindani wa aina yoyote lazima apatikane mshindi na mwingine ushindwa hii ni kanuni ya ushindani hivyo ndivyo ilivyo, na kwa kanuni hiyo hiyo CCM ilishinda kwa kura nyingi. Kwa mara nyingine tena tunakupongeza.
Mh. Raisi Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, baada ya kazi nzuri yenye matunda uliyoifanya katika kipidi cha awamu ya kwanza ya uongozi wako tunakutakia afya njema katika kuliongoza Taifa letu kipindi cha pili cha uongozi wako wa miaka mitano ijayo. Tunaomba Mwenyezi Mungu akuongoze na akusaidie kulinda na kutetea dhamana kubwa uliyo kabidhiwa na wananchi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.


KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI


Mwenyekiti wa CCM
Tawi la Moscow Dr. Alifred Kamuzora

No comments: