CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Tuesday, February 22, 2011

SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKA TAWI LA CCM MOSCOW-URUSI KWA WALIOPATWA NA MAAFA GONGOLAMBOTO JIJINI DAR-ES-SALAAM


TAWI LA CCM MOSCOW-URUSI
SALAAM ZA RAMBIRAMBI KWA WALIOPATWA NA MAAFA  GONGOLAMBOTO JIJINI DAR-ES-SALAAM
Uongozi na Jamii nzima ya Tawi la CCM Moscow na vitongoji vyake nchini Urusi kwa masikitiko makubwa  umepokea taarifa ya maafa yaliyotokea sehemu za Gongolamboto jijini Dar-Es-Salaam, baada ya milipuko mikali ya silaha za kijeshi katika Ghala la kuhifadhia silaha hizo. Tukio hilo ilimechukua maisha ya watanzania wenzetu katika hali isiyotemewa. Msiba huu ni wa Watanzania wote bila kujali itikadi dini au vyama vya siasa. Huu ni msiba wa Taifa zima, hivyo tunaungana na Watanzania wote popote walipo kuwafariji  wote waliopoteza jamaa, ndugu na marafiki zao na tupo nao katika msiba huu mzito na tunaungana nao kuwaombea marehemu Mwenyezi Mungu aziweke roho za walipoteza maisha yao mahali pema peponi Amin.
Kwa wale waliopo hospitalini tunawaombea wapone haraka na warejee na afya njema, tunaamini kabisa Mwenyezi Mungu atawajalia afya njema, na tunaamini kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua za haraka kabisa iwezekanavyo kuakikisha huduma za muhimu zinapatikana kwa wote waliopatwa na maafa hayo.
Vile vile kwa kuamini juhudi za uongozi wa serikali yetu tunaamini itachukua hatua madhubuti katika kutafuta chanzo cha maafa yaliyotokea na kutoa mwongozo madhubuti katika utaratibu wa kuifadhi zana hizi muhimu za kijeshi, ili tukio kama ili lisitokee tena. Pamoja na hayo uchunguzi wa kina ufanyike kama ikionekana kuna uzembe ambao uliweza kusabisha maafa haya basi wahusika wachukuliwe hatua na wawajibishwe.
Hivyo watanzania wote tuungane kuwaombea wote waliopoteza maisha Mwenyezi Mungu awalaze roho zao mahali pema peponi. Amin


Mwenyekiti Tawi
Dr. Alfred Kamuzora

No comments: