CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Wednesday, May 4, 2011

UCHAGUZI WA VIONGOZI WA CCM TAWI LA MOSCOW

UCHAGUZITANGAZO
Chama cha Mapinduzi Tawi la Moscow kinapenda kuwafahamisha wanachama wake wote kuwa kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa tawi. Nafasi zitakazogombaniwa;
1. Mwenyekiti wa Tawi
2. Katibu wa Tawi
3. Katibu wa siasa na uenezi wa Tawi
4. Katibu wa uchumi na fedha wa Tawi
5. Mwenyekitti UVCCM
6. Mwenyekiti UWT (Umoja wa Wanawake)
7. Katibu UVCCM
8. Katibu UWT
9. Katibu wa Fedha UVCCM
10. Katibu wa Fedha UWT
11. Katibu wa siasa na uenezi UVCCM
Kwa mwanachama yeyote yule anayetaka kugombea nafasi za 1-4 zilizotajwa hapo juu, fomu zinapatikana kwa katibu wa tawi Neema Charles Kengese block 9 chumba namba 1404 A kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni. Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 20 May 2011. Uchaguzi utafanyika tarehe 28 May 2011, muda na mahali mtafahamishwa.
Kwa yeyote anayetaka kugombea nafasi yoyote UVCCM awasiliane na Katibu wa UVCCM Mahamoud O. Mbarouk email mosmbarouk@yahoo.com na UWT wasiliana na Katibu wa UWT Odilia Kasiga. Uchaguzi wa UVCCM na UWT ni lazima ufanyike kabla ya tarehe 15.05.2011. Kuanzia tarehe 16.05.2011 uteuzi kwa nafasi ambazo zitakuwa wazi utaanza rasmi. Wote mnaombwa kutoa ushirikiano wa dhati ili kufanikisha zoezi hili.


UTARATIBU WA KUGOMBEA KWA KIFUPI
• Mwanachama yeyote wa CCM anaweza kugombea nafasi yoyote ya CCM. Ili kugombea nafasi yoyote ya UVCCM ni lazima uwe na kadi ya UVCCM na UWT ni lazima uwe mwanachama wake. (Wakinadada wote wenye kadi ya CCM wanaruhusiwa kugombea au kupiga kura UWT) Wapigakura wa UWT wanaweza kupiga kura UVCCM
• Kupiga kura ni kwa kutumia kadi ya CCM na kwa wale wanaUVCCM ni kwa kutumia kadi zote mbili yaani kadi ya CCM na ya UVCCM
• Kwa wale watakaogombea nafasi yoyote UVCCM hawataweza kugombea nafasi yoyote UWT. Hivyo hivyo kwa wale watakaogombea nafasi yoyote UWT hawataweza kugombea nafasi yoyote UVCCM


KAMATI YA UCHAGUZI
1) Bi. Neema C. Kengese - Katibu na mkurugenzi mkuu wa uchaguzi
2) Bw. Salimu Mfungahema – Katibu wa siasa, itikadi na Uenezi na Mkurugenzi mkuu msaidizi wa uchaguzi
3) Bw. Boniface Assenga – Katibu wa uchumi na fedha na Uenezi na Mkurugenzi mkuu msaidizi wa uchaguzi


Kwa maelezo zaidi tembelea ccmmoscow.blogspot.com au facebook.com/ccmmoscow


Aksanteni sana
Tuendelee kupeperusha bendera ya CCM nje ya nchi.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI,


Bi. Neema C. Kengese
Katibu na mkurugenzi mkuu wa uchaguzi
Tawi la CCM
Moscow - Russia

No comments: