Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mhe.Mwigulu Lameck Nchemba juzi tarehe 31 Oktoba 2013 alifunga rasmi mafunzo ya UVCCM ambayo yalifanyika kwa muda wa wiki mbili. Mafunzo hayo ambayo yalifanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya Namtumbo yakihusisha vijana wote wa UVCCM kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Ruvuma yalikuwa na madhumuni ya kuwajengea vijana hao uwezo wa kutambua umuhimu wao katika jamii ikiwa ni pamoja na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika nchi yetu, kujua siasa za nchi yetu pamoja na namna ya kufanya maamuzi sahihi wakati huu wa ujana. Mafunzo hayo yalilenga pia kuwaandaa vijana hao kifikra na kimaadili kwaajili ya kupokea na kuendeleza jukumu muhimu la kukijenga na kukiimarisha chama chetu CCM pamoja na jumuiya zake zote, na hasa jumuiya ya vijana, UVCCM.
Mhe. Mwigulu Nchemba akivishwa skafu na kijana wa UVCCM mara baada ya kuwasili kwenye kambi ya mafunzo ya vijana wa CCM wilayani Namtumbo. |
Naibu Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na vijana hao wakati wakiwasili eneo la tukio |
Vijana wakiwa na furaha kuonana na kusalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mhe.Mwigulu Nchemba |
Mhe.Mwigulu Nchemba akizungumza na vijana hao wakati wa kufunga mafunzo hayo. |
Mhe. Naibu Katibu Mkuu akitoa kadi ya uanachama wa UVCCM kwa mmoja wa vijana wa CCM walioshiriki mafunzo hayo |
Mhe. Mwigulu Nchemba akimtununu mmoja wa vijana wa UVCCM cheti cha kuthibitisha kuwa ameshiriki mafunzo hayo |
Mhe. Mwigulu Nchemba akisalimiana na mmoja kati ya wazee wa CCM wilayani Namtumbo |
Mbunge wa Namtumbo Mhe. Vita Kawawa akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Mwigulu Nchemba |
Mhe. Mwigulu Nchemba akiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Namtumbo |
Mhe. Naibu Katibu Mkuu wa CCM akipatiwa maelewo kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM wa wilaya ya Namtumbo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya kisasa ya CCM wilayani hapo |
Mhe. Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mhe.Mwigulu Nchemba akisaini katika kitabu cha wageni katika ofisi ya CCM wilayani Namtumbo |
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mhe.Mwigulu Nchemba akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Said Mwambungu |
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mhe.Mwigulu Nchemba alipomtembelea Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mhe. Abdulla Lutavi ofisini kwake. |
No comments:
Post a Comment