Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alirejea nyumbani Tanzania jana tarehe 02 Novemba akitokea nchini Uingereza alikokwenda kwa ajili ya kuhudhuria mkutano mkuu wa kimataifa wa Serikali Uwazi (OPEN GOVERNMENT PARTNERSHIP SUMMIT).
Mkutano huo ambao ulijadili masuala ya uwazi katika serikali na ushirikiano kati ya serikali na wadau mbalimbali nje ya serikali, ulifanyika jijini London kuanzia tarehe 31 Oktoba 2013 mpaka tarehe 1 Novemba 2013.
|
Mhe. Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa JKN, Dar-es-Salaam jana taree 2 Oktoba. Aliyeongozana naye ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam na pia Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mwantumu Mahiza |
|
Mhe. Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwa ameongozana na Mhe. Makamu wa Rais Dkt Mohamed Bilali pamoja na viongozi wengine wa serikali waliofika uwanjani hapo kumpokea |
|
Mhe. Rais akisalimiana na viongozi mbalimbali wa serikali na wakuu wa majeshi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar-es-Salaam. |
No comments:
Post a Comment