Matembezi ya mshikamano yaliyofanywa na wanachama wa chama cha mapinduzi jana tarehe 2 Februari huko Jijini Mbeya wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za kumbukumbu ya miaka 37 tangu kuzaliwa Chama cha Mapinduzi - CCM.
Matembezi hayo ya umbali wa kilomita tano yalifanyika kuanzia saa moja na nusu mpaka saa mbili na robo, kutoka katika viwanja vya Soweto kwenda Bustani ya uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
|
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akibadilishana mawazo na Naibu wake(Bara) Ndg.Mwigulu Nchemba wakati wakimsubiri Mwenyekiti wa CCM , Mhe. Rais Jakaya Kikwete kuwasili eneo la Soweto jijini Mbeya ili kuanza matembezi ya mshikamano wakati wa kuadhimisha miaka 37 ya CCM. |
|
Mwenyekiti wa CCM - Taifa Ndg Jakaya Kikwete akiteta jambo na watoto kabla ya kuanza matembezi. |
|
Askari wa usalama barabarani na usalama wa Mhe. Rais wakijiweka tayari kuupanga msafara wa matembezi hayo. |
|
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza matembezi hayo huku akiwa na watoto ambao aliwateua kutembea nao baada ya kuwaona eneo la Soweto. |
|
Mwenyekiti wa CCM, Ndg. Kikwete akiwapungia mkono wananchi matembezi yalipoanza eneo la Soweto. Wengine kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Kinana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Ndg. Godfrey Zambi |
|
Mpiga picha wa Mhe. Rais , Anko Michuzi (shati jeupe), akiwajibika. |
|
Matembezi yakiendelea. |
|
Wakazi wa Jijini Mbeya wakiwa katika shamrashamra za matembezi hayo. |
|
Wafanyabiashara katika soko lililopo karibu na Uwanja wa Sokoine,wakimpungia mkono Mwenyekiti wa CCM, Ndg. Jakaya Kikwete wakati akipita pamoja na wananchi katika eneo hilo wakati wa matembezi hayo. |
|
Mwenyekiti wa CCM, Ndg. Jakaya Kikwete akiwasli kwenye Bustani ya Uwanja wa Sokoine yalikokomea matembezi hayo. |
|
Mwenyekiti wa CCM Ndg. Jakaya Kikwete kulia akiingia kwenye bustani ya jiji la Mbeya tayari kwa kupokea matembezi hayo yaliyoanzia Soweto Mwanjelwa na kumalizikia katika bustani hiyo kiasi cha umbali wa kilomita tano. kutoka kushoto ni Katibu wa NEC Fedha na Uchumi Mama Zakhia Megji, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana , Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi. |
|
Wana-CCM na wananchi kwa jumla wakimlaki Rais Kikwete kwenye Bustani ya Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. |
|
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Ndg. Nape Nnauye akihamasisha wakati Mwenyekiti wa CCM, Ndg. Jakaya Kikwete alipowasili kwenye Bustani ya Uwanja wa Sokoine mwishoni mwa matembezi hayo |
|
Ndg. Sixtus Mapunda akiwasalimia wananchi. |
|
Mbunge wa Rungwe Mashariki, Profesa Mark Mwandosya akikaribishwa na Ndg. Nape kusalimia wananchi mwishoni mwa matembezi hayo. |
|
Mwenyekiti wa CCM, Ndg. Jakaya Kikwete akiwa amepumzika na viongozi wenzake baada ya kuwasili kwenye bustani ya Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya baada ya matembezi hayo. |
|
Mwenyekiti wa CCM Ndg. Jakaya Kikwete akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia pamoja na Katibu wa NEC Oganizesheni, Dr. Mohamed Seif Khatibu huku, wakifurahia mazungumzo hayo. |
|
Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe akizungumza na wananchi, kulia ni Ndg. Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi. |
|
Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi mwishoni mwa matembezi hayo. |
|
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) , Ndg. Philip Mangula akiwasalimu wananchi mwishoni mwa matembezi hayo. |
|
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndg. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wana Mbeya mara baada ya kupokea matembezi hayo kwenye bustani ya Jiji jijini Mbeya ikiwa ni maadhimisho ya miaka 37 ya Chama cha Mapinduzi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Sokoine jana jijini Mbeya. |
No comments:
Post a Comment