CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Tuesday, February 4, 2014

MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM YALIYOFANYIKA KITAIFA JIJINI MBEYA

Sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi zilizofanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya tarehe 2, Februari, zikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM - Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama pamoja na maelfu ya wananchi.

Mwenyekiti wa CCM, Ndg. Jakaya  Mrisho Kikwete, akiwasili katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya kuwaongoza wana-CCM katika kilele cha maadhimisho ya miaka 37 ya CCM

Mwenyekiti wa CCM Ndg. Jakaya Kikwete akisalimiana na  Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sokoine.

Mwenyekiti wa  CCM Ndg. Jakaya Kikwete akizungumza jambo  na  Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sokoine, Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula.

Mwenyekiti wa  CCM Ndg. Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wana CCM  na wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo.

Mwenyekiti wa CCM Ndg. Jakaya Kikwete akiendelea kusalimia wananchi kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 

Ndg. Jakaya Kikwete akionesha kwa furaha kubwa alama ya CCM ya jembe na nyundo ambayo aliichukua kwa mmoja wa mashabiki wa CCM walioingia nayo Uwanjani hapo.

Vijana 37 wakirusha juu njiwa 37 ikiwa ni ishara ya CCM kutimiza miaka hiyo. 

Gwaride la chipukizi likitoa heshima kwa Mwenyekiti wa CCM Ndg. Jakaya Mrisho Kikwete.

Chipukizi wakila kiapo cha Utii kwa Chama.

Katibu Mkuu wa CCM , Ndg. Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Ndg. Jakaya Kikwete kuhutubia wanachama pamoja nawananchi waliojitokeza kuhudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mwenyekiti wa CCM , Ndg. Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wanachama wa CCM pamoja na wananchi katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Umati wa watu waliohudhuria uwanjani  hapo.

Mwenyekiti wa CCM Ndg. Jakaya Kikwete akikabidhi bajaji kwa mmoja wa walemavu ambaye alimuahidi kumpatia bajaji hiyo. 

Wasanii wa filamu na muziki wa kizazi kipya waliojiunga na CCM siku hiyo, wakishangilia baada ya kutambulishwa na Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Ndg.Nape Nnauye kwenye sherehe hizo.

Ndg. Jakaya Kikwete akimkabidhi kadi ya uanachama wa CCM Irene Uwoya mara baada ya kujiunga na chama hicho.

Mwigizaji wa filamu Jacob Steven JB akizungumza kwa niaba ya wenzake kabla  ya waigizaji hao wa Bongo Movie kukabidhiwa kadi zao na Rais Jakaya Kikwete katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Ndg. Jakaya Kikwete akipiga picha ya pamoja na wasanii waigizaji wa filamu mara baada ya kuwakabidhi kadi zao kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya

Mwigizaji maarufu wa filamu nchini , Irene Uwoya akiwa amezongwa na mashabiki wake katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Wasanii wa Filamu na muziki wa kizazi kipya wakicheza kwa furaha baada ya kutangazwa kuwa watapewa kadi za CCM na Mwenyekiti wa CCM, Ndg. Jakaya Kikwete katika sherehe hizo

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Ndg. Nape Nnauye akishiriki kucheza ngoma ya kinyakyusa wakati wa sherehe hizo.

Moja ya kundi la TOT ndogo likitumbuiza katika sherehe hiyo.

Ndg. Nape pamoja na Ndg. Sixtus Mapunda (Katibu Mkuu UVCCM) , wakicheza muziki uliokuwa unapigwa na kundi la TOT wakati wa sherehe hizo.

Khadija Kopa akitunzwa na mashabiki alipokuwa akitumbuiza pamoja na kikundi cha TOT wakati wa sherehe hizo.

Ndg. Nape Nnauye (kulia) , Ndg. Sixtus Mapunda Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa pamoja na Kada wa CCM Bw. Mawakipesile(kushoto) wakiserebuka na wanachama wengine wa CCM katika maadhimisho hayo.

Ndg. Kinana akisoma toleo maalumu la gazeti la Mzalendo wakati akiwa katika sherehe hizo.

Ofisa wa Uhuru Publications Limited, akiwaga gazeti la Mzalendo kwa wasanii wa filamu na muziki.

Wasanii wakisoma gazeti la Mzalendo wakati wa sherehe hizo.

Banda la UHURU/Mzalendo katika viwanja vya Sokoine jijini Mbeya.

No comments: