CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Sunday, February 23, 2014

WAZIRI MKUU Mhe. MIZENGO PINDA AFUNGUA SEMINA YA JUMUIYA YA WAZAZI NGAZI YA TAIFA , MKOANI DODOMA JANA

Jana Tarehe 22 Februari , 2014, Mhe. Peter Mizengo Pinda alifungua semina ya viongozi na watendaji wa Jumuiya ya Wazazi (CCM), ngazi ya Taifa, mikoa na wilaya. Ufunguzi wa semina hiyo ulifanyika katika ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM - Taifa, mjini Dodoma.

Mhe. Mizengo Pinda akihotubia wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwa ukumbini wakati semina ikiendelea
Mhe. Pinda (kushoto) akiongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Ndg. Abdallah Majura Bulembo(kulia),  Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya,  Bi. Dogo Idd Mabrouk (wa pili kushoto), na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi, Ndg. Mohammed Seif Khatib (wa pili kulia), wakitoka ukumbini baada ya kufungua semina hiyo.
Mhe. Pinda akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Ndg. Abdallah Majura Balembo(kulia), Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya  Ndg. Mohammed Seif Khatib(wa pili kulia), Makamu Mwenyekiti Bi. Dogo Idd Mbrouk (wa tatu kulia), na Mjumbe mwingine wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo Mhe. Adam Malima (kushoto). 

No comments: