CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Monday, March 31, 2014

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM - TAIFA,
Ngd. ABDULRAHMAN KINANA,
KATIKA MIKOA YA RUKWA, KATAVI NA KIGOMA


Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana jana Machi 30, 2014 alianza ziara yake ya kutembelea wananchi wa mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma. Katika ziara hiyo ya siku 21, Ndg. Kinana atakagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, pia atazungumza moja kwa moja na wananchi kuhusu kero mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kujadiliana nao njia mbalimbali za kutatua kero hizo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndg.Abdulrahman Kinana akishuka kwenye Ndege, katika Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga jana Machi 30, 2014, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku 21 katika mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Ndg.Hypolitus Matete, akimlaki Ndg.Kinana (kulia) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga, jana. Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa, Bi.Lahel Ndegeleke.
Ndg. Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa CCM mkoani Rukwa, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga, jana.
Ndg. Kinana akisalimiana na wananchi mbalimbali waliofika kumlaki katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga, jana.

PIA JANA HIYO JUMAPILI, MACHI 30, 2014 Ndg. KINANA ALIFANYA MKUTANO WA HADHARA NA WANANCHI WA MJI MDOGO WA NAMANYERE ULIOPO WILAYANI NKASI, KATIKA MKOA WA RUKWA.

Katibu Mkuu wa CCM, Ndg.Abdulrahman Kinana akisalimiana na kikundi cha kinamama wa hamasa, mara baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika, Jumapili, Machi 30, 2014, katika mji mdogo wa Namanyere, wilayani Nkasi, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kizitatua, katika mkoa wa Rukwa.
Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia mamia ya wananchi katika mkutano huo uliofanyika katika mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa, jana Jumapili, Machi 30, 2014.
Kijana Elias Yeremia akimuuliza swali Ndg. Kinana jukwaani, katika mkutano huo wa Namanyere, Nkasi mkoani Rukwa.
Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume akihutubia mkutano huo wa Namanyere.
Baadhi ya vijana wa Namanyere wakiwa wamepanda juu ya lori na wengine wakiwa wamesimama pembeni huku wakimsikiliza kwa makini Ndg. Kinana kwenye mkutano huo wa Namanyere.
Wazee wakimsikiliza Ndg. Kinana katika mkutano huo wa hadhara.
Mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wa hadhara.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Ndg.Hypolitus Matete, akimshukuru Ndg. Kinana kwa hotuba nzuri, katika mkutano huo wa Namanyere.
Kikundi cha matarumbeta kikitoa burudani kwenye mkutano huo wa Ndg.Kinana na wananchi wa mji mdogo wa Namanyere, mkoani Rukwa.
Mzee Rogas Nkana akimpatia Ndg Kinana ushahidi wa vielelezo na nyaraka mbalimbali kuhusu mirathi ya binti yake ambayo ameifuatilia kwa muda mrefu hadi sasa bila mafanikio. Mzee Nkana alidai mbele ya Ngd.Kinana kwamba madai hayo kwa ajili ya mirathi ya kifo cha binti yake ambaye alifariki dunia mwaka 2000 akiwa mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani katika Jeshi la Uhamiaji yamekuwa kitendawili licha ya kufuatilia katika ofisi husika kwa muda mrefu. Mzee Nkana alipata fursa hiyo wakati Ngd.Kinana alipoamua kukutana na waasisi wa Chama cha Mapinduzi pamoja na mabalozi kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali katika ukumbi wa Community Centre katika mji mdogo wa Namayere wilayani Nkasi, katika mkoa wa Rukwa.

No comments: