CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Tuesday, April 1, 2014

KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI NKASI, MKOANI RUKWA


Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa wenyeji wake kuhusiana na hatua za awali za ujenzi wa bandari ya Kabwe, wilayani Nkasi, mkoani Rukwa.
Mmiliki wa Kampuni ndogo ya kusindika samaki Bw. Nassor Shibib akimpa maelezo mafupi Ndg. Kinana kuhusu namna ya kuhifadhi samaki aina ya migebuka kabla ya kusafirishwa na wafanyabiashara wa eneo hilo na kuuzwa katika nchi za Zambia, Congo, Burundi na Rwanda.
Ndg. Kinana akipata maelezo mbalimbali kuhusiana na suala la uvuvi katika eneo hilo ambalo linatarajiwa kujengwa bandari.
Ndg. Kinana akiangalia samaki aina ya migebuka katika kiwanda kidogo cha kuhifadhia samaki hao, kijijini Kabwe katika wilaya ya Nkasi.
Samaki aina ya migebuka ikiwa imeandaliwa kwaajili ya kukaushwa kabla ya kuhifadhiwa kwenye majokofu na kusafirishwa maeneo mbalimbali, ndani na nje ya nchi.
Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, Mhe. Ally Keisy alipokwenda kukagua ujenzi wa bandari ya Kabwe ambao uko katika hatua za awali, na kujionea shughuli mbalimbali za uvuvi zinazofanyika katika kijiji hicho cha Kabwe.
Ndg. Kinana akishiriki katika ujenzi wa Ofisi ya CCM katika kijiji cha Kabwe, wilayani Nkasi, mkoani Rukwa.
Ndg. Kinana akiwahutubia wananchi na wanachama wa CCM, jana , katika kijiji cha Kabwe, wilayani Nkasi. Aliwahakikishia wananchi hao kuwa Serikali inatambua matatizo yao likiwemo suala la pembejeo za kilimo, maji pamoja na uvamizi wa wavuvi.
"Miradi yote inayotekelezwa nchi nzima kwa sasa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010, hatubagui kwa kuwa wote ni watanzania ..." alisema Ndg.Kinana. Pia aliongeza kuwa Serikali inatambua vizur kuwa shughuli kubwa kijijini hapo ni uvuvi, hivyo itajitahidi kuwe na utaratibu wa kuwasaidia kupata mikopo ili waweze kununua zana za uvuvi kusudi waweze kujiendeleza.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kirando, wilayani Nkasi mapema jana. Ndg. Kinana alisema kuwa atahakikisha barabara ya kutoka Sumbawanga mjini kwenda kijiji cha kwabwe inatengenezwa kwa kiwango cha lami. "Nitaenda kwa mbunge wenu kushinikiza suala la barabara jii ili ijengwe kwa kiwango cha lami na kuwarahisishia shughuli za kibiashara ..." alisema. Pia aliongeza kuwa ... maendeleo hayawezi kuja ikiwa miunombinu ni mibovu hivyo, atahakikisha analifikisha suala hilo kwa waziri mwenye dhamana pamoja na mkuu wa nchi ili kazi hiyo ifanyike mapema.


No comments: