CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Wednesday, April 2, 2014

RIDHIWANI AENDELEA NA KAMPENI YA UBUNGE KATIKA KIJIJI CHA TOKAMISASA, JIMBONI CHALINZE

Mgombea ubunge katika jimbo la Chalinze
kwa tiketi ya CCM
Ndg. Ridhiwani Kikwete.
  • Jana , Aprili 1, 2014, Ndg. Ridhiwani aliendelea na kampeni yake ya kujinadi kwa wananchi wa kijiji cha Tokamisasa, jimboni Chalinze.
  • Awaahidi wananchi wa Tokamisasa kuwa ataanza na Barabara, kisha elimu, afya pamoja na kurudisha michezo jimboni humo.
  • Pia awaahidi kuhakikisha anamaliza tatizo la mgogoro kati ya wakulima na wafugaji kwa kuweka mipango bora ya matumizi ya ardhi kijijini hapo.

Ndg.Ridhiwani Kikwete akihutubia wakazi wa kijiji cha Tokamisasa wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge zinazoendelea jimboni Chalinze.
Ndg. Ridhiwani akihutubia wakazi wa kijiji cha Tokamisasa.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ndugu Ridhiwani Kikwete akicheza muziki na Miraji Mtaturu, Katibu wa CCM  Wilaya ya Mufindi wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge jimbo la Chalinze uliofanyika kwenye kitongoji cha Mbuyu kijiji cha Tokamisasa kata ya Ubena Zomozi.
Msanii Sam wa Ukweli akitumbuiza kwenye kampeni za CCM zilizofanyika katika kijiji cha Tokamisasa kitongoji cha Mbuyu.
Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ndugu Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wazee wa kijiji cha Tokamisasa wakati akiwasili kwenye kitongoji cha Tuka Mjini tayari kwa kufanya mkutano wa kampeni.
Msanii wa Mashairi Mwanahamisi Mohamed wenye ulemavu wa macho akiimba shairi linaloitwa Changamoto wakati wa mkutano wa CCM wa kampeni za ubunge jimbo la Chalinze.
Wakina Mama wa Kimasai wakifuatilia kwa makini mkutano wa kampeni za ubunge za CCM ambapo Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mgombea ubunge kwa tiketi ya  CCM ) alifika katika tawi la Kivuga na kuomba kura.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi - CCM, Ndg.Nape Nnauye akizungumza na wafugaji wa Kimasai wa Tawi la Kivuga kata ya Ubena Zomozi wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge jimbo la Chalinze.
Ndg. Ridhiwani Kikwete akizungumza na vijana wajasiriamali wa UVCCM mshikamano Visakazi mara baada ya kuzindua shina hilo lililopo katika kata ya Ubena Zomozi.
Ndg. Ridhiwani akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Tokamisasa, kata ya Ubena Zomoni wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika jana Aprili 1, 2014 jimboni Chalinze.
Mgombea ubunge katika jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ndg. Ridhiwani Kikwete akishiriki kucheza mziki na wananchi wa kitongoji cha Mbuyu, katika kijiji cha Tokamisasa, kata ya Ubena Zomoni, wakati wa muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za ubunge iliyofanyika jana Aprili 1, 2014.

 

No comments: