CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Tuesday, April 8, 2014

RIDHIWANI KIKWETE ASHINDA KWA KISHINDO JIMBONI CHALINZE

Ngd. Ridhiwani Kikwete
Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Ngd. Ridhiwani Kikwete ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha nafasi ya ubunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani.

Katika uchaguzi huo mdogo uliofanyika Aprili 6, 2014, CCM imepata ushindi wa asilimia 86.53 ikiwa ni sawasawa na kura 20,812. Vyama vingine vilivyoshiriki uchaguzi huo ni pamoja na Chadema waliopata asilimia 10.92 ambayo ni sawasawa na kura 2,628, CUF wamepata asilimia 1.92 sawasawa na kura 473. APF kimepata asilimia 0.32 sawasawa na kura 78, huku NRA kimepata asilimia 0.24 sawasawa na kura 59.

Uchaguzi huo mdogo umefanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Marehemu Saidi Bwanamdogo, ambaye alifariki Januari mwaka huu.


No comments: