CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Wednesday, April 14, 2010

Salamu za Rambirambi


YAH: SALAMU ZA RAMBIRAMBI , KIFO CHA RASHIDI MFAUME KAWAWA..
Kwa niaba ya Kamati ya Siasa ya Tawi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, Tawi la Mosow Urusi, nachukua nafasi hii kukutumia Salamu za Rambirambi Kwako Wewe Mheshimiwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kupitia Kwako, ningependa kutoa Salam za Rambirambi kwa Familia ya Hayati Rashidi Mfaume Kawawa (Simba wa Vita) na kwa WatanzaniaWote.
Watanzania tumepoteza kiungo na jemedari wa kutumainiwa kwa mambo mengi. Hayati Kawawa alikuwa mtu mtaratibu , makini sana na muungwana mambo yalimfanya awe kipenzi cha wengi. Chama Cha Mapinduzi Kimepoteza Kiongozi na Kada mkongwe mahiri aliye kuwa na sifa zisizokuwa na kifani. Familia Yake imepoteza Baba mpenzi, Mlezi na Nguzo ya kutegemewa.
Kifo cha Mheshimiwa Hayati Rashid Mfaume Kawawa kimetokea wakati ambapo alikuwa anahitajika sana na Watu wa rika zote ;"Kifo Chake kimewagusa na kuwasikitisha watu wengi ndani na nje ya Tanzania.
Wengi Wetu tutamkumbuka Mheshimiwa Hayati Kawawa kwa mchango wake muhimu Serekalini, ndani ya CCM na katika Jamii. Alikuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya Wanachama wa CCM na Watanzania wote kwa ujumla.
Maisha yake hapa Duniani yamefikia mwisho, lakini mawazo na busara Zake zitaendelea kuwepo daima na milele ndani ya jamii ya Watanzania na hasa Vijana.“Kwa wanafamilia , alikua ni Mlezi na Mzazi na kwa watanzania alikua ni Mlinzi wa kukidhimatarajio ya baadae kwa vijana hasa katika midani ya Siasa.”
Kwa moyo wa dhati na majonzi makubwa , tunaungana na Familia ya Hayati Kawawa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Tunaelewa machungu waliyonayo wanafamilia, lakini tunapenda kuwahakikishia kwamba machungu hayo sio yao peke yao bali ni ya Watanzania wote. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na kuwafariji.
Tunatambua kabisa kuwa maamuzi yake Mola na kazi yake daima haina makosa.Sisi sote tulimpenda sana ila Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi na kumtwaa kwenye ufalme wake.
"Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili aiweke Roho Yake Mahali Pema Peponi.
Amina!
Dr. Alfred Kamuzora
MWENYEKITI TAWI -CCM MOSCOW

No comments: