CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Wednesday, July 27, 2011

TUMETHUBUTU ,TUMEWEZA, na TUNASONGA MBELE.

 Nape Nnauye akiwa anahutubia Mkutano wa hadhara Mbeya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti uwanjani hapo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa na Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sita,Christopha Ole Sendeka mbunge wa jimbo la Simanjiro pamoja na Dr.Harrison Mwakyembe mbunge na Naibu Waziri wa Ujenzi na Miundombinu walisema kuwa azma yao ya kupambana na mafisaji bado ipo pale pale.
 
’Ndugu zangu Nyoka akijivua gamba ni kweli sumu huongezeka lakini pia ngozi yake huwa nyororo na anaweza kukimbia vizuri na sumu ambayo imeongezeaka CCM ni kuwabaini na kuwaondoa waovu wote ndani ya chama na Serikali kwasababu watendaji wa Serikali ni wauza duka linalomilikiwa na CCM’’ alisema Nape.
 
Aidha, alikemea tabia za wauguzi wanaowatukana akina mama wajawazito wanapoenda kujifungua kwa kuwatamkia maneno ya kejeri, Polisi wanaogeuza matatizo ya wanaopelekwa vituoni kuwa biashara kwao na maofisa watendaji wa Vijiji na kata wanaotaka fedha wakati wa kusaini fomu za dhamana na nyaraka mbalimbali zikiwemo zile za mikopo ya vyuo vikuu.

Kwa upande wake Mbunge Samwel Sitta aliongeza kuwa hawatanyamaza kamwe hadi pale watakapo hakikisha dhana ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Jakaya Kikwete  ya ‘kujivua gamba’ inakamilika kwa wale wote ambao hawako safi ndani ya chama hicho kwa kuachia madaraka waliyonayo ndani ya chama na Serikali kwa manufaa ya chama na wananchi kwa ujumla, huku akisahau kuwa aliwahi kumkejeli Rais Kikwete na kumwambia kuwa anapaswa kuongeza ukali kidogo katika maamuzi yake.

“Wakati tunapiga kelele bungeni kuhusu mafisadi mimi na wenzangu,baadhi ya wenzetu walituchukia sana na kujenga chuki dhidi yetu kiasi cha wengine kutaka kuninyang’anya kadi ya chama lakini nilisimama imara na leo tunayaona matunda” alisema Sita.

Dr. Mwakyembe alisema kuwa wananchi hasa wanachama wa CCM wanapaswa kuwapuuza wale wote wanaosema kuwa Serikali imeshindwa kuchukua maamuzi magumu na kwamba maamuzi magumu yanaweza kufanywa na watu wasiokuwa na hekima wakiwemo vibaka na Majambazi.

‘’Maamuzi magumu yanafanywa hata na vibaka lakini Serikali ya awamu ya Nne inafanya maamuzi Sahihi na makini’’ alisema Dr. Mwakyembe huku akitafsiliwa kuwa ni majibu dhidi ya Mbunge wa Jimbo l Monduli Edwar Lowasa ambaye hivi karibuni amenukuliwa akisema kuwa Serikali iliyopo madarakani inaumwa ugonjwa wa kutochukua maamuzi magumu.
Alisema kuwa, Rais alipoona baadhi ya viongozi wanaenda  kinyume na matakwa ya waasisi wa chama hicho,ndipo alipoamua kuanzisha dhana hii ili kurudisha sura nzima ya CCM ya zamani ambayo ilikuwa ikiwajali wakulima na wafanyakazi masikini,hivyo tuna kila sababu ya kutembea kifua mbele katika kulisimamia hili.

Mkutano huo Ulioanza kwa MAANDAMANO na UMATI MKUBWA ulihudhuriwa pia na Wabunge wa CCM mkoani hapa, Wenyeviti, makatibu na wajumbe wa ngazi zote kutoka matawi na Kata zote pamoja na wilaya  zinazounda mkoa wa Mbeya ambapo jumla ya wanachama  497 wamepokelewa na kurudisha kadi huku wanachama wapya 2689 wakijiunga na chama hicho na wengine 300 kutoka vyuo vikuu vilivyopo mkoani hapa wakijiunga na chama hicho.

No comments: