CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Monday, August 22, 2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI YA SIASA ,TAWI-CCM MOSCOW :21/8/2011, MOSCOW -URUSI

Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya tawi la CCM Moscow-URUSI imemaliza kikao chake cha siku moja, jioni ya tarehe 21/08/2011 mjini Moscow chini ya Uenyekiti wa Kaimu Katibu wa Tawi, Ndg  Bakunda C.D. Pamoja na mambo mengine Kamati ya siasa ya tawi  imeamua yafuatayo;

1. Kamati ya siasa ya tawi imepokea  taarifa ya kiutendaji ya tawi kwa mwaka wa 2010/11 iliyowasilishwa na  Katibu wa halmashauri kuu, itikadi na Uenezi wa Tawi Ndg KOLOWA.K.M na  kupitisha kalenda ya vikao vyote vya tawi kwa mwaka 20111/12 ambapo kalenda  hiyo inaanza kutekelezwa 1/9/2011. Aidha Kamati ya siasa ya tawi inatoa wito kwa WAJUMBE wa Vikao vyote vya tawi na vya Jumuiya, wana CCM, wapenzi na wakereketwa wa hapa URUSI kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha kalenda iliyopitishwa inazingatiwa.Taarifa za Kiutendaji ya tawi inapatikana kupitia website ya tawi ccmmoscow.blogspot.com. au katika facebook   “chama cha mapinduzi-ccm”
2 Kamati ya siasa imepokea na kuridhia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa katibu wa fedha na uchumi wa Jumuiya ya Vijana ya tawi na Mjumbe wa kamati ya maadili ya Tawi akiwakilisha Jumuiya ya Vijana,Bi Maria Semeni Festo. Aidha Kamati ya Siasa imempongeza kwa uamuzi huo uliozingatia maslahi mapana ya chama chake na Tawi kwa Ujumla. 
3. Aidha Kamati Kuu imejadili masuala mengine ya kijamii na kuwataka watanzania kudumisha Nidhamu zao huku Ugenini na kujikita ktka kuitangaza Tanzania katika nyanja mbalimbali (michezo, utamaduni,na Kuzingati ELIMU). Aidha Kamati ya Siasa  ya tawi inachukua fursa hii kumpongeza Barozi wa Tanzania nchini Urusi Kepten Mstaafu JAKA MWAMBI ,na watendaji wote wa Ubalozi, pamoja na mambo mengine,  kwa juhudi zao za kuwasaidia watanzania hapa urusi na Kuimarisha mkakati wa kuitangaza  Tanzania kupitia Maonyesho ya Utamaduni wa mwafrika yaliofanyika hivi karibuni jijini Moscow pamoja na majukumu mengine walionayo kwa taifa katika eneo lao la Uwakilishi.
 4. Kamati ya Siasa ya Tawi imejadili kwa kina Vipaombele vya Tawi kwa mwaka 2011/12 na  kupitisha kwa kauli moja,kama ifuatavyo :
(a)Uboreshaji wa Mfuko wa tawi kupitia njia mbadala za Ukusanyaji wa vyanzo vya uchumi kupitia jumuiya za tawi
(b)Uzingatiwaji wa Ukusanyaji wa ada za uanachama kupitia kila Jumuiya za tawi na utoaji wa Risiti kwa kila mwanachama hai kwa mwaka 2011/12
(c) Mpango mkakati wa kuongeza wanachama wa tawi na ufunguzi wa SHINA jipya la  watanzania wana-CCM ktk  Mji wa TURA-URUSI. Ufunguzi wa shina hilo jipya unatarajia  kufanyika October.
(d). Jitihada Endelevu za kuwa na MLEZI wa Tawi la CCM Moscow . Kamati ya Siasa ya tawi imemteua aliyekuwa katibu wa Tawi Ndg Boniphace Thomas Assenga kuwa Kiongozi wa JOPO la wajumbe watakaosimamia mchakato wa mawasiliano na  Mlezi wa Tawi CCM MOSCOW na Sekretariet ya CCM ,huko Dar es salaam -Tanzania.
(e) Kuimarishwa kwa jitihada za kimawsiliano na matawi mengine ya CCM yalio nje ya Tanzania ktk lengo la kufahamiana na kubadilishana uzoefu kiutendaji, Matawi hayo ni UK, USA na ITALY.
(f) Maandalizi ya Mpango Mkakati wa Tawi katika kusheherekea Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara
5. Kamati ya siasa ya tawi imeipongeza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Tawi kwa kazi nzuri  na kuitaka iongeze kasi katika utekelezaji wa majukumu yake, ili kuhakikisha mageuzi yaliyokusudiwa yanatekelezwa kwa wakati.
6. Kuhusu suala la maadili ndani ya tawi, Kwa kuzingatia taarifa fupi iliyowasilishwa na  Mjumbe wa Kamati ya Maadili ya tawi  Ndg Manda Iddy Shaaban “Tawi kwa kufuata maagizo ya Chama litaendelea kusimamia maadili, na kuwataka wale waliotakiwa kujipima na kuwajibika watumie muda huo, kujipima na kuwajibika kwa masilahi mapana ya chama na tawi.”
Kamati ya siasa ya tawi imeipa kamati ya maadili muda wa wiki mbili zaidi  iwe imekamilisha report  ya jukumu iliyopewa na  kuwakilisha mapendekezo yake katika kikao kitakachofuata.
Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Tawi inatarajiwa kukutana wakati wowote kipindi cha mwezi Septemba-December 2011 kulingana na agizo la kalenda ya Vikao vya tawi, ambapo pamoja na mambo mengine itatathimini utekelezaji wa maamuzi yake.                                                                              
                  Imetolewa na kuthibitishwa;                   
KOLOWA. K. M.
KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZI
TAWI CCM MOSCOW-URUSI

No comments: