CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Monday, August 22, 2011

TAARIFA YA SEKRETARIETI KUU TAWI LA CCM-MOSCOW MWAKA 2010/2011

Ifuatayo ni taarifa ya sekretarieti kuu ya tawi la ccm-moscow URUSI.Taarifa hii ina vipengele vifuatavyo:-

UTANGULIZI
Kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kunipa nafasi hii kutoa taarifa ya utekelezaji na mwelekeo wa chama cha mapinduzi katika tawi letu  hili hapa MOSCOW URUSI katika kikao hiki halali kwa mujibu wa kanuni za chama chetu CCM.
Ndugu wajumbe, kamati ya siasa ya tawi ambayo inahusisha wajumbe 12 tuliopo katika kikao hiki leo napenda kutoa taarifa hii mbele yenu ikiwa na ishara ya wazi kuwa demokrasia katika tawi letu na hata katika jumuiya zetu zilizopo katika  tawi la ccm MOSCOW imekomaa vizuri na inaendelea kukuzwa na mijadala mbalimbali katika mikutano endelevu ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa ujumla.

Ndugu wajumbe: Chama cha mapinduzi tangu kimeanzishwa hapa Moscow urusi kilikuwa na mikakati mbalimbali ya kichama ili kuweza kuhakikisha kuwa tawi linakuwa imara na hatimaye kuzidi kuimarisha chama kwa ujumla.vilevile napenda kusema kutokana na sera na itikadi za chama cha mapinduzi kwa kufuata katiba ya chama na taratibu tulizojiwekea katika chama ni msingi pekee tunajivunia kama chama cha mapinduzi  katika kulinda na kutetea haki na maslahi ya chama kitaifa kwa pamoja.Mbali na jukumu hilo pia ni wajibu wa chama kusaidia wananchi kuelewa serikali yao kuwa inafanya kitu gani  katika kuleta maendeleo ya taifa na hatimaye kuweza kupambana na adui mkubwa wa maendeleo katika nchi yetu ambae ni umaskini.

MAFANIKIO
Ndugu wajumbe wa kamati ya sias:,  kiutendaji na katika kutekeleza majukumu ya chama cha mapinduzi katika tawi letu kumekuwa na mafanikio mbalimbali na makubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa tawi la chama cha mapinduzi Moscow.Haya yote ni katika kutekeleza majukumu ya chama cha mapinduzi tangu kilipoanzishwa.

A.KUPATIKANA KWA WANACHAMA WAPYA.
Chama cha mapinduzi tawi la mocsow limeweza kupata  idadi ya wanachama wapya kwa idadi ya kuridhisha sana kutokana na matokeo mazuri ya wanachama hao kuhamasishwa kwa kiasi cha kutosha na kupelekea kuijiunga na  chama cha mapinduzi tawi(CCM-MOSCOW) hii ikimaanisha kwamba nyongeza hiyo ya wanachama imepelekea tawi kuwa na idadi ya wanachama 97 kwa kipindi cha mwaka 2010/11.Vile vile jumuiya mbalimbali za ccm tawi Moscow zimeweza kuhamasisha na kuwa na idadi kubwa ya wanachama katika jumuiya hizo.Hivyo basi napenda kutoa pongezi kwa jumuiya zote mbili kwa kazi nzuri waliofanya na wanayoifanya mpaka sasa kuhakikisha chama kinakuwa na wanachama wengi kuanzia ngazi ya tawi mpaka kwenye jumuiya zake.Napenda kusema kuwa mafanikio haya hayakupatikana hivi hivi bali  kutokana na shughuli mbalimbali tulizoweza kuzifanya kupitia tawi na jumuiya zake kwa ujumla.Kwa mfano sherehe mbalimbali zilizofanyika kwa kipindi tofauti tofauti za kichama na jumuiya zimeweza kuhamasisha watu wengi kujiunga kutokana kazi nzuri tunayoifanya katika tawi.Hivyo basi napenda kutoa ombi kupitia tawi zoezi hili tunalolitumia mara kwa mara la sherehe katika kuhamasisha watu liwe endelevu,ingawa naamini kuwa uhamasishaji wa mtu mmoja mmoja  upo lakini sio wa kutosha sana ikilinganishwa na sherehe.

B.MAWASILIANO KATIKA TAWI.
Ndugu wajumbe wa kamati ya siasa: chama cha mapinduzi tawi la MOSCOW-URUSI limeweza kuimarisha mawasiliano mazuri kwa ukaribu zaidi kupitia uongozi wa tawi na jumuiya zake  hivyo kupelekea tawi kujulikana  zaidi kitaifa na kimataifa katika matawi mengine yaliyopo ndani na nje ya nchi ya Tanzania.Kwa kipengele hiki cha mawasiliiano napenda kutoa pongeza kwa mwenyekiti wa tawi  Dr.Kamuzora kwa kazi nzuri anayoifanya katika kuhakikisha chama cha mapinduzi tawi la MOSCOW-URUSI linafahamika zaidi kutokana na safari mbalimbali anazozifanya akiwa nyumbani Tanzania na kuweza kupita katika ofisi mbalimbali kitaifa na  kutufikishia ujumbe wa uwepo wa tawi la CCM- Moscow-urusi na hivyo tawi kupewa kipaumbele zaidi.Vilevile pongezi hizi sio tu kwa Dr.kamuzora pia hata kwa viongozi wengine katika chama wanaojituma katika kuhakikisha mawasiliano ya chama katika Nyanja mbalimbali yanapalekea tawi la CCM MOSCOW-URUSI kufahamika zaidi.Kwa mfano jumuiya ya wanawake na jumuiya ya vijana katika tawi zinafahamika sana kutokana na mawasiliano mazuri yaliopo na  yanayoimarishwa  katika jumuiya hizo kupitia viongozi wake na hivyo basi kupelekea chama kufahamika  zaidi pamoja na jumuiya zake ndani na nje ya Tanzania.Hivyo basi napenda kutoa ombi kuwa uimarishwa mzuri wa mawasiliano katika chama na jumuiya uwe wa hali ya juu na upewe  kipaumbele cha kutosha katika kuimarisha tawi letu.

C.MATATIZO.
Pamoja na kuwa na mafanikio katika chama cha CCM MOSCOW-URUSI,pia na  jumuiya zake kimekuwa kinakabiliwa na matatizo mbalimbali na hivyo kuchangia kurudisha nyuma maendeleo ya tawi letu katika utekelezaji wa dhamira na malengo mbalimbali ya chama katika tawi.Matatizo hayo ni kama ifuatavyo:-
1.MIGOGORO.
Ndugu wajumbe wa kamati ya siasa,chama cha mapinduzi katika tawi kimekuwa kinakabiliwa na migogoro mingi sana ya mara kwa mara katika nyadhifa za viongozi wa juu wa tawi na kusababisha kuondoa matumaini kwa wanachama tunaowaongoza na viongozi wengine kwa ujumla.Hali hii imesababisha watu wengi kutopenda kujiunga na chama kutokana na migogoro ambayo iko wazi na ambayo ilikuwa ikiendelea mara kwa mara ndani ya chama katika tawi.

 2.NIDHAMU NA MAADILI.
 Ndugu wajumbe wa kamati ya siasa,nidhamu na maadili katika chama imeshuka kwa kias kikubwa sana.Hali hii imechangiwa sana  kwa viongozi na  wanachama  kutokuheshimiana    viongozi kwa viongozi kutokuheshimiana na hivyo kusababisha nidhamu na maadili katika chama.Kutokana na kushuka huku kwa nidamu na maadili katika chama imesababisha kuondoa matumaini na uaminifu wa wanachama kwa viongozi na vilevile kuondoa uaminifu wa kiongozi katika utendaji wake katika chama.Katika kipengele hiki cha nidamu na maadili natoa ombi kwa viongozi wote kuwa nidhamu na maadili lazima vipewe kipaumbele kwa viongozi wote na wanachama kwa ujumla ili kuweza kuimarisha tawi.Vile vile napenda kuipa nafasi kamati ya nidhamu  na maadili kuchukua hatua zake kikamilifu katika katika kuhakikisha nidhamu na maadili kwa viongozi inachukuliwa hatua za haraka pale inapo onekana kuwa kiongozi ameshindwa kuendana na taratibu ambazo chama cha mapinduzi imejiwekea.Kumbuka kamati ya nidhamu na maadili ni mhimili mkubwa sana kwa chama cha mapinduzi hivyo ni chombo pekee kinachohakikisha nidhamu na maadili ya viongozi katika chama inafuatwa na kutekelezwa.

 3.KUSHINDWA KUKAMILISHA MALENGO YA TAWI.
 Ndugu wajumbe wa kamati ya siasa,chama cha mapinduzi tawi la Moscow limeshindwa      kutimiza malengo yake mengi tu ambayo tuliyapanga katika kipindi cha mwaka 2010/11 ikiwa ni pamoja na kushindwa  kufanya sherehe za kuhamasisha watu kujiunga na chama cha mapinduzi Moscow vilevile na kushindwa kufanya ziara ambazo tulitaka kuzifanya kutembelea miji mingine nje ya Moscow katika kuhamasisha na kufungua mashina sehemu hizo.Hii yote imesababishwa na  migogoro iliyokuwepo  katika chama na kupelekea viongozi kukaa vikao kutatua matatizo ya migogoro hiyo na kuacha kufanya shughuli za kimaendeleo katika kuimarisha chama na kutanua tawi katika sehemu nyingine nje ya Moscow.Vilevile chama katika tawi kimeshindwa kuimarisha mfuko wa tawi hivyo kusababisha tawi kutegemea jumuiya katika kuendesha shughuli zake za kichama zaidi.hivyo basi basi natoa pendekezo katika kipindi hiki cha uongozi mwaka 2011/12 naomba chama kijikite katika kuboresha mfuko wa chama na kutimiza malengo yote tutakayojipangia katika kipindi hiki cha uongozi.Hivyo ni jukumu la kila kiongozi na mwanachama katika kuhakikisha malengo yote tutakayoyapanga yanatimia kuanzia ngazi ya tawi na jumuiya zake kwa ujumla.

D.MAPENDEKEZO
Ndugu wajumbe wa kamati ya siasa,chama cha mapinduzi CCM MOSCOW-URUSI kupitia kamati ya sekretarieti kuu inapenda kutoa mapendekezo yake kama ifuatavyo:-
·         Ushikiano wa viongozi na wanachama kwa ujumla uwe wa uakribu zaidi katika tawi na jumuiya pia ili kuweza kufikia malengo tuliojipangia katika tawi.Hili litakuwa changamaoto nzuri sana ambayo itawezesha viongozi kufanya kazi vizuri na kwa ari na ngumu moja.
·         Kuepuka migogoro na migongano katika tawi na jumuiya ambayo sio ya lazima kwa viongozi wake na wanachama.Hili tukiliondoa katika chama basi kila kiongozi atakuwa anafanya kazi kwa ufanisi kutokana na nafasi yake katika tawi au jumuiya.Na vile vile kusabisha wanachama kuamini utendaji wa kiongozi katika chama.
·         Suala la kuwajibika kwa kila kiongozi lazima lipewe kipaumbele ili kuweza kufikia malengo na mataraji tuliyojiwekea kataka tawi.Kiongozi anatakiwa kuwajibika kutokana na nafasi yake alionayo ili kuweza kutambua mchango wake katika nafasi hiyo kwa kuweza kushirikiana na viongozi wenzie.Hii itatuwezesha kufanya utekelezaji wa majukumu mbalimbali tuliyonayo katika nafasi ya tawi na jumuiya kwa ujumla.
·         Suala la nidhamu na maadili kwa viongozi  linahitaji kusimamiwa kwa ukaribu zaidi kwa kupitia kamati ya nidhamu ili kuweza kulifanya tawi letu na chama kwa ujumla kuwa mfano bora wa kuigwa na matawi mengine ndani na nje Tanzania.

E.VIPAUMBELE:
Ndugu wajumbe wa kamati ya siasa,sekretarieti kuu ya chama katika tawi kupitia vikao vyake viwili ilivyofanya na wajumbe wa kamati hiyo kutoka jumuiya mbalimbali imetoa vipaumbele vifuatavyo:-
·         1)Uboreshaji wa mifuko ya  tawi na jumuiya zote  zijikite katika kuinua mifuko hiyo katika nyanja mbalimbali.
·         2)Ada ya uanachama katika tawi na jumuiya pia zipewe kipaumbele katika makusanyo yake.
·         3) Upande wa kutunisha mifuko njia mbadala elekezi za kukuza mifuko hiyo katika tawi na jumuiya.
·         4)Wajumbe wa Vikao vyote vya CCM au jumuiya wanatakiwa kuvaa sare za Chama.
·         5)Ongezeko la wanachama lazima litiliwe kipamumbele.
·         6)Kufanyika uchaguzi wa viongozi wa tawi mwaka 2012 kulingana na kalenda ya chama
·          7)Jitihada  zifanyike katika kupata mlezi wa tawi.
·         8)Jitihada zifanyike ili kuweza kuwasiliana na matawi mengine ya nje ya nchi.
·          9) Mkakati wa tawi wa kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.
 
F. HITIMISHO
Ndugu wajumbe wa kamati ya siasa mwisho napenda kuchukua nafasi hii kwa kutoa shukarani zangu kwa  kuweza kunisikiliza kwa umakini zaidi kuhusu taarifa hii ya sekretarieti ya chama tawi ambayo inatakiwa kupitishwa na halimashauri kuu ili iweze kwenda kwa wanachama kwa ajili ya kutoa mtazamo na dira ya chama cha mapinduzi tawi la Moscow siku ya mkutano mkuu wa wanachama wote.Asanteni sana kwa kunisikiliza kwa makini naamini yale yaliyomo katika taarifa hii na kuweza kuyasikiliza kwa umakini naamini kila kiongozi atayabeba na atayafanyia kazi vya kutosha ili kuweza kukuza demokrasia ya taifa na utawala bora kwa serikali yetu ya Tanzania.
                                                                                                                                                               
                                                                    ASANTENI

                                                               KOLOWA.K.M                                              21/8/2011
                                    KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZAJI TAWI
                                                        

No comments: