JUMUIYA YA UMOJA WA VIJANA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) TAWI LA MOSCOW –
URUSI KWA KUSHIRIKIANA NA UONGOZI WA TAWI NA WANACHAMA WAKE KWA UJUMLA
UNAPENDA KUWATAKIA HERI YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN WAISLAM WOTE KOKOTE
PALE DUNIANI.
KATIKA SALAMU HIZO UONGOZI WA JUMUIYA UKIONGOZWA NA
MWENYEKITI WAKE UNAPENDA KUWAASA WAISLAM KUTUMIA FURSA HII ADHIMU YA
MWEZI HUU AMBAO UNA FAIDA NYINGI NA MALIPO YA ZIADA KATIKA IBADA ZAKE NA
KAMA ILIVYOANISHWA KATIKA MAFUNDISHO KUWA NI MWEZI AMBAO WAJA
WATAZIDISHIWA REHMA ZA MOLA WAO KWA KUTENDA AMALI NJEMA,WATAKUWA NA
FURSA YA KUPEWA MSAMAHA NA MOLA PAMOJA NA KUACHWA HURU NA ADHABU YA MOTO
SIKU YA KIAMA.
UVCCM UNAWATAKIA MFUNGO MWEMA WA MWEZI WA
RAMADHAN NA INSHAALLAH MWENYEZI MUNGU AWE NI MWENYE KUZIPOKEA NA
KUZIKUBALI SWAUM ZAO NA KUWALIPA MALIPO STAHIKI KAMA ALIVYOAHIDI KATIKA
KITABU KITUKUFU CHA QURAN.
IMETOLEWA NA MWENYEKITI
UVCCM – MOSCOW - URUSI
No comments:
Post a Comment