CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Tuesday, July 16, 2013

SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA MSIBA WA NDG. DISMAS MATHIAS KAJOGOO

UONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA MOSCOW NCHINI URUSI, KWA MASIKITIKO MAKUBWA UNATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA NDUGU DISMAS MATHIAS KAJOGOO  ALIYEFARIKI ALFAJIRI YA LEO TAREHE 16 JULAI 2013, AMBAPO HADI UMAUTI UNAMFIKA ALIKUWA NI MMOJA KATI YA MAAFISA WA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI URUSI.
NDUGU DISMAS KAJOGO AMBAYE AMEFIKWA NA UMAUTI AKIWA AMELAZWA HOSPITALI NCHINI URUSI AMBAPO ALIKUWA AKIENDELEA NA MATIBABU KWA MARADHI YALIYOKUWA YAKIMSUMBUA. CCM-MOSCOW KWA PAMOJA INATUMA SALAMU ZA POLE KWA FAMILIA YAKE YOTE , NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WOTE WA MAREHEMU POPOTE PALE WALIPO NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA KUFUATIA MSIBA HUO.
KWA PAMOJA TUNAAMINI NA KUKUBALI KUWA HAKIKA HILI NI PENGO KWA WATANZANIA WOTE WALIOPO NCHINI URUSI NA NCHI JIRANI AMBAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE HUHUSIKA NA UTENDAJI WA OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI URUSI, NA TAIFA LETU LA TANZANIA LAKINI HATUNA BUDI KUSEMA KUWA TUACHE MAPENZI YA MUNGU YATIMIE KWANI YEYE NDIYE MMILIKI WA KILA KITU HAPA DUNIANI NA KESHO AKHERA.
TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AIPOKEE ROHO YA MZEE WETU NA AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI. KWAKE TUMETOKA NA KWAKE NI MAREJEO JINA LA MUNGU LIHIMIDIWE AMEEN .

TAARIFA HII IMETOLEWA NA UONGOZI WA TAWI CCM - MOSCOW

1 comment:

Anonymous said...

Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani. Amen