CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Monday, October 14, 2013

TAARIFA YA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM TAWI MOSCOW

Halmashauri kuu ya CCM tawi la Moscow - Urusi ilifanya kikao tarehe 05 Oktoba 2013.

Katika kikao hicho mwenyekiti wa Tawi Dr. Alfred Kamuzora aliwataka viongozi wa Tawi kuwa na mwamko wa kutekeleza maazimio ya tawi. Viongozi walikubaliana kulinda na kueneza sera za Chama kwa pamoja.


Pamoja na hayo Dr. Kamuzora ametoa changa moto kwa viongozi wenzake kwamba Tawi linatakiwa lijiendeshwe, kwa pamoja viongozi wote kwa kauli moja wamekubaliana kutafuta vyanzo mbali mbali vya kuendesha tawi na kuwa na uwezo wa kusaidia watoto wenye mazingira magumu waishio Tanzania. Katika hoja hiyo Dr. Kamuzora alisema ni busara kutoa msaada wa hali na mali hili litakuwa jambo la busara kusaidi watoto waishio katika mazingira magumu huu utakuwa mchango mkubwa kwa Taifa, maana watoto watakao saidiwa ni taifa la kesho.

Mwenyekiti amesema Tawi litakuwa tayari kushirikiana na wale wote ambao wanapenda kuleta maendeleo ya nchi kupitia Tawi, watapokelewa na tutashirikiana nao maana moja ya malengo ya Tawi hili ni pamoja na kusaidia kutangaza nchi yetu kwa  kutekeleza maazimio na ahadi za Chama Taifa. Hivyo mwenyekiti amesema ni vema kutangaza nchi yetu kupitia Tawi na sehemu zingine ambazo zinaweza kuwa na mwanya kwa kutangaza jina la nchi yetu kupitia utamaduni na Lugha yetu ya Kiswahili. 

Sisi lazima kuendeleza harakati za kuleta maendeleo nchini kwetu bila kujari itikadi maana sisi ni mabalozi wa nchi moja na tufanye kazi ya kuletea maendeleo ya Taifa letu kwa kutafuta wawekezaji  na wataalam katika nyanja mbali mbali na hasa zile ambazo zitaongeza  msukumo wa haraka wa maendeleo ya Taifa letu.

Katika kikao hicho mwenyekiti alipendekeza kuwa ni muda muafaka kusimamia kauri mbiu za chama kama zilivyo ainishwa kwenye ilani ya uchaguzi , akiongeza mwenyekiti alisema sehemu kubwa ya  maazimio yametekelezwa hii  ni kutokana na uongozi mahili wa Mwenyekiti wa Chama Taifa ambaye ni Raisi wa Jamuhuri ya muungano Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kama alivyosema Mwenyekiti wa ChamaTaifa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ni wajibu wa viongozi wa chama na selikari kubainisha mafanikio ya maazimio ya  Chama kwa wananchi. Viongozi wana wajibu wa kuwaambia  wananchi wetu nini kimefanyika katika mikoa, wilaya na mpaka vijijini katika nchi yetu.

Dr. Kamuzora aliendelea kwa kusema ni siku chache, katika hotuba yake makini Raisi Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amezidi kuudhihilishia umma kwamba ni kiongozi mahili kwa busara zake katika maamuzi magumu yaliyojaa busara na hekima katika mchakato mzima wa mabadiliko ya katiba, ni kwa busara na hekima zake zimezidi kuleta amani na mshikamano wa taifa letu.

IMETOLEWA NA UONGOZI WA TAWI MOSCOW.

No comments: