CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA MOSCOW –
URUSI, KINAUNGANA NA WATANZANIA WOTE POPOTE WALIPO KUADHIMISHA MIAKA
14 TANGU TULIPOONDOKEWA NA BABA WA TAIFA , MWALIMU JULIUS KAMBARAGE
NYERERE TAREHE 14 OKTOBA 1999.
DAIMA TUTAENDELEA KUMKUMBUKA MWALIMU
AMBAYE ALIKUWA MFANO BORA KWETU KAMA KIONGOZI HODARI NA MCHAPA KAZI,
ALIYEPIGANIA UHURU WA MWAFRIKA, ALIYEPIGANIA HAKI SAWA KWA WOTE NA
KUCHUKIA UKANDAMIZAJI WA MASKINI WANYONGE, KIONGOZI AMBAYE ALIICHUKIA
SANA KUIPIGA VITA RUSHWA, KIONGOZI AMBAYE ALIJITOLEA KUPIGA VITA
UJINGA, MARADHI, NA UMASKINI KATIKA NCHI YETU.
WATANZANIA NA WAAFRIKA TUTAENDELEA
KUMKUMBUKA MWALIMU KWA NAMNA ALIVYOSHIRIKIANA NA VIONGOZI WENZAKE
BARANI AFRIKA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKOLONI NA HASA UKOMBOZI WA
NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA, KATIKA JITIHADA ZA KUWAUNGANISHA WAAFRIKA
ILI WAWE NA NGUVU YA PAMOJA DHIDI YA WANYONYAJI NA WAKOLONI, NA PIA
JITIHADA ZAKE KATIKA KUTATUA MIGOGORO MBALIMBALI ILIYOKUWA
IKIHATARISHA AMANI NA UTULIVU KATIKA NCHI MBALIMBALI AFRIKA NA HASA
UKANDA WA MAZIWA MAKUU.
SIKU YA LEO TUNAPOMKUMBUKA MWALIMU
NYERERE, WATANZANIA TUKUMBUKE KUENZI MAISHA YAKE PIA IKIWA NI PAMOJA
NA KUYAISHI KWA MATENDO YALE MAZURI YOTE AMBAYO MWALIMU ALITUFUNDISHA
NA KUTUACHIA.
TUENDELEE KUPIGANIA AMANI UMOJA NA
MSHIKAMANO WETU, HASA KATIKA WAKATI HUU AMBAPO TAIFA LETU LIKO KATIKA
MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA AMBAYO NDIYO TAA NA MWONGOZO WA
TAIFA LETU.
CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA MOSCOW –
URUSI KINAWATAKIA WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA YENYE AMANI NA
UTULIVU.
"UPUMZIKE KWA AMANI MWALIMU"
IMETOLEWA NA UONGOZI , TAWI LA CCM
MOSCOW – URUSI.
No comments:
Post a Comment