Tarehe 15 Oktoba 2013 , Mhe, Rais Jakaya Kikwete alifanya mkutano na viongozi wa vyama vya siasa nchini vyenye uwakilishi bungeni. Mkutano huo uliofanyika Ikulu, Dar-es-Salaam ulihudhuriwa na Mhe. Freeman Mbowe (Mwenyekiti - CHADEMA), Mhe. Profesa Ibrahim Lipumba (Mwenyekiti - CUF), Mhe. James Mbatia (Mwenyekiti - NCCR-Mageuzi), Mhe. Nancy Mrikaria ( aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP, Mhe. Augustine Mrema), Mhe. Isaack Cheyo (aliyemwakilisha Mwenyekiti wa UDP, Mhe. John Cheyo) na Mhe. Philip Mangula (Makamu Mwenyekiti - CCM)
Pia wengine waliohudhuria ni pamoja na Mhe. William Lukuvi (Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge), Mhe. Steven Wassira (Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu), Mhe. Mathias Chikawe (Waziri wa Katiba na Sheria), waheshimiwa Tundu Lissu na John Mnyika kutoka CHADEMA, Bw. Martin Mng'ong'o kutoka NCCR-Mageuzi, pamoja na Mhe. H. Mnyaa na Bwana Julius Mtatiro kutoka CUF.
Mhe. Rais alikubaliana na viongozi hao mambo yafuatayo:
Kwanza, kwamba vyama vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba viwasilishe mapendekezo yao haraka Serikalini ili itafutwe namna ya kuyashirikisha mapendekezo hayo katika marekebisho ya Sheria hiyo.
Pili, kwamba vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa Katiba mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano kwa pamoja vitakavyosukuma mbele mchakato huo kwa maslahi mapana ya nchi yetu na mustakabali wa taifa. Hivyo basi, Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kilipewa jukumu la kuratibu jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa vyama hivyo na wadau wengine nchini.
Wakati mkutano ukiendelea Ikulu, Dar-es-Salaam |
Video fupi ya Mhe. Rais Jakaya Kikwete akiwa na Viongozi wa vyama vya siasa na wasaidizi wao, Ikulu - Dar-es-Salaam.
IMETOLEWA NA UONGOZI, TAWI LA CCM MOSCOW - URUSI
IMETOLEWA NA UONGOZI, TAWI LA CCM MOSCOW - URUSI
No comments:
Post a Comment