CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Thursday, October 17, 2013

TAARIFA YA UJIO WA NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MJUMBE WA BARAZA LA WADHAMINI CCM , Dr. CHARLES TIZEBA

Tarehe 12.10.2013 Naibu Waziri wa Uchukuzi Dr. Charles Tizeba ambaye alitembelea Jiji la Moscow nchini Urusi kikazi, alipata fursa ya kukutana na Mwenyekiti wa Tawi la CCM - Moscow, Dr.Alfred Kamuzora ambaye aliambatana na Naibu Katibu wa Siasa na Uenezi - Tawi, ndugu Salim Mfungahema pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha wa Tawi, Bi. Hilda Kifanga.

Katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa na wadau mbalimbali pia, Naibu waziri alifafanua masuala mbalimbali yakiwemo, utendaji wa wizara yake katika kufikia matokeo makubwa na ya haraka(big results now). alifafanua maeneo mbalimbali ambayo yametekelezwakatika mpango huo na ambayo yapo kwenye utekelezaji.

Pia Naibu Waziri aliwataka watanzania waishio nchuni Urusi wafuatilie kwa umakini Mchakato mzima wa Rasimu ya Katiba Mpya ili waweze kuifahamu vizuri na baadae waweze kutoa maono kwa usahihi sahihi.

Katika mkutano huo Mwenyekiti wa Tawi la CCM - Moscow , Dr. Afred Kamuzora alipata fursa ya kuzungumza mambo machache kuhusu Tawi la CCM - Moscow, pamoja na mambo mengine alibainisha kuwa ipo haja ya serikali  inayoongozwa na CCM kuongeza kasi ya kuondoa kero za wananchi kwa wakati ili kufikia malengo ya matokeo makubwa na ya haraka. Pia Dr. kamuzora alisema kwamba kitendo hicho kitapelekea CCM kujihakikishia  nafasi kubwa zaidi ya ushindi katika uchaguzi ujao mwaka 2015.

Naibu Naibu Katibu wa Siasa na Uenezi Ndg. Salim Mfungahema wakati akitoa maoni yake katika kikao hicho alisema kuwa umefika wakati sasa Chama Cha Mapinduzi kuongeza nguvu zaidi katika kuimarisha matawi yake ya nje kwani mengine yanahitaji kuongezewa nguvu kutokana ukweli kuwa wanachama wake wengi ni wanafunzi wa elimu ya juu.

IMETOLEWA NA UONGOZI, TAWI LA CCM MOSCOW - URUSI

No comments: