Dr. Charles Tizeba ( Naibu Waziri wa Uchukuzi ) |
Katika kikao kifupi na viongozi wa Tawi mwenyekiti amemuelezea naibu waziri Dr. Tizeba kuwa ni kiongozi mahili kwani ni kiongozi ambaye mahali popote yupo tayari kukitetea na kukilinda chama kwa kila hali. Huu ni ujasiri ambao ametuachia sisi kama viongozi wa Tawi kusimamia itikadi na sera za chama mahali popote na wakati wowote.
Dr. Kamuzora alisema kuwa Dr. Charles Tizeba ambae ni Naibu Waziri wa Uchukuzi ni mfano wa kiongozi wa kuigwa kwani ni kiongozi asiyependa urasimu kwani ni muwazi na mtendaji na ambae anakubali kusikiliza na kutoa ushauri na uamuzi pale ambapo uamuzi huo unatakiwa kutolewa na yale yakufanyia kazi basi anayatolea maelezo. Hii ilibainishwa katika mkutano ambao Naibu Waziri aliufanya alipokutana na watanzania pamoja na maofisa wa ubalozi wa watanzania jijini Moscow nchini Urusi.
Wakati huo huo Dr. Kamuzora amewataka viongozi wa Tawi kuiga mifano ya viongozi kama hawa wenye ujasili na wasiopenda urasimu kama ilivyoonekana kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi Dr. Charles Tizeba.
IMETOLEWA NA UONGOZI, TAWI LA CCM MOSCOW
No comments:
Post a Comment