CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Friday, November 15, 2013

RAIS KIKWETE AWASILI NCHINI SRI LANKA KWA AJILI YA KUHUDHURIA MKUTANO WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA

Rais wa Jamhuri ya muungano wa tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasili jijini colombo, sri lanka jana alhamisi , Novemba 14, 2013 kuhudhuria mkutano wa wakuu wa serikali za nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CHOGM). Katika safari hiyo rais kikwete ameambatana na mkewe mama Salma Kikwete pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

Mkutano huo ambao utaanza rasmi leo ijumaa, Novemba 15, 2013 jijini Colombo utafunguliwa na Prince Charles (mtoto wa malkia wa Uingereza) kwa niaba ya mama yake Malkia Elizabeth (ambaye ndiye kiongozi wa Jumuiya ya Madola), kwa kuwa Malkia Elizabeth hatoweza kuhudhuria mkutano wa mwaka huu.

Jumuiya ya Madola inaundwa na nchi zilizokuwa chini ya ukoloni na himaya ya Uingereza na nchi nyingine ambazo ziliomba na hatimaye kujiunga na jumuiya hiyo kama vile Msumbiji na Rwanda. Jumuiya hiyo ina jumla ya wanachama 53, zikiwemo nchi 18 kutoka bara la Afrika, nchi 8 kutoka bara la Asia, nchi 13 kutoka Marekani na “Caribbean”, nchi 3 kutoka Ulaya na nchi 11 kutoka “Pacific”.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bandaranaike, mjini Colombo Sri Lanka na Mheshimiwa Chandrasiri Gajadeera, Waziri wa “Rehabilitation and Reforms” wa nchi hiyo wakati alipowasili jana asubuhi nchini Sri Lanka

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri wa “Rehabilitation and Reforms” wa Sri Lanka Bwana Chandrasiri Gajadeera, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bandaranaike huko Colombo

Rais Jakaya Kikwete akiambatana na Mkewe Mama Salma kwenda kutia saini kwenye kitabu cha wageni mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Bandaranaike nchini Sri Lanka

Rais Jakaya Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa ngoma za kitamaduni mara baada ya kuwasili jijini Colombo

Rais jakaya kikwete na mke wake mama Salma Kikwete wakiongea na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue mara baada ya kuwasili jijini Colombo , Sri Lanka , jana novemba 14, 2013 tayari kwa mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola (CHOGM)

No comments: