CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Sunday, November 24, 2013

TAWI LA CCM MOSCOW LAMPONGEZA WAZIRI BENARD MEMBE

Mhe. Benard Membe
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mwenyekiti wa Tawi la CCM Moscow Dr. Alfred Kamuzora, kwa niaba ya Tawi, amempongeza Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Benard Membe, kwa kuteuliwa kuongoza kamati yenye nguvu ya Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Madola (CMAG) katika mkutano uliofanyika nchini Sri Lanka wiki iliyopita. 

Hii ni ishara madhubuti ya kuonyesha jinsi gani kiongozi huyo alivyo makini na amekubalika kwa kuamininiwa kuongoza chombo hicho, ambacho ni kamati pekee yenye mamlaka ya kuisimamisha uanachama nchi  yoyote ndani ya Jumuiya ya Madola. Hii imetuongezea sifa kama Taifa katika bara la Africa na duniani kote. 

Mwenyekiti wa CCM
Tawi la Moscow
Dkt. Alfred Kamuzora
Waziri Benard Membe amekuwa ni mwafrika wa kwanza kuchukua madaraka hayo katika miaka ya hivi karibuni na kupewa kwake nafasi hiyo inadhihirisha kukomaa kwa viongozi na nchi yetu ya Tanzania katika  uongozi wa juu wa kidiplomasia ambayo Tanzania imeufikia. 

Tawi la Chama Cha Mapinduzi Moscow limepokea taarifa hiyo ya kuteuliwa Waziri Membe kwa furaha, heshima na taadhima. Viongozi vinara watazidi kupeperusha bendela ya Taifa letu daima popote ulimwenguni na watazidi kutujengea imani na heshima ya nchi yetu.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

No comments: