Dr. Asha-Rose Migiro |
Rais, Dk. Jakaya Kikwete amemteua Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Maifa (UN) Mstaafu, Dk. Asha-Rose Migiro kuwa Mbunge.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, imesema, Uteuzi huo ambao umetangazwa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, ulianza tangu Desemba 2, 2013.
Dk. Asha-Rose Migiro kwa sasa ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anayesimamia Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI).
Akizungumzia uteuzi huo juzi, akiwa Mbalizi mkoani Mbeya, Dk. Asha-Rose amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi, akisema ameupokea kwa furaha, na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment