CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Monday, December 16, 2013

CCM TAWI LA MOSCOW - URUSI PAMOJA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI URUSI WASHEREHEKEA SIKUKUU YA UHURU WA TANGANYIKA

Baadhi ya wanachama wa CCM Tawi la Moscow pamoja na watanzania wengine katika picha ya pamoja
Siku ya Jumamosi ya tarehe 14 Desemba, 2013 wanachama wa CCM tawi la Moscow – Urusi waliungana na watanzania wengine waishio nchini Urusi kusherehekea siku ya Uhuru wa Tanganyika. Sherehe hiyo ilifanyika tarehe 14 Desemba kutokana na muingiliano wa siku halisi ya Uhuru wa Tanganyika (9 Desemba) kuingiliana na ratiba ya kimasomo, ikizingatiwa kuwa wanachama wengi wa tawi ni wanafunzi, na hivyo kupelekea maadhimisho ya sherehe hiyo kusogezwa mbele.

Sherehe hiyo ambayo ilifana sana ilihudhuriwa pia na raia wa nchi jirani za Afrika Mashariki na baadhi ya marafiki ambao raia kutoka nchini Urusi, ambao walikuja kuwapongeza watanzania na jirani zao kwa kupata uhuru.

Katika sherehe hiyo ya kuadhimisha miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika, mwenyekiti wa CCM tawi la Moscow, Dkt.Alfred Kamuzora wakati akiongea na watanzania pamoja na wageni waalikwa aligusia mambo kadha wa kadha yanayogusa mustakabali wa nchi yetu. Ikizingatiwa kuwa Afrika na dunia nzima iko kwenye maombolezo ya msiba wa Rais wa Kwanza mweusi wa Afrika Kusini Hayati mzee Nelson Mandela (Madiba), Dkt.Kamuzola aliwaasa watanzania na viongozi kuishi maisha ya kuthaminiana, kutokupenda visasi na chuki kwa maadui kama alivyoishi mzee Mandela. Pia viongozi kutokupenda kung’ang’ania madaraka, kutekeleza na kujali demokrasia. Mambo ambayo yalimfanya Mzee Mandela kuwa tofauti na viongozi wengine wengi dunia.

Akizungumzia kuhusu tawi la CCM – Moscow, Mwenyekiti Dkt.Kamuzora alisisitiza yafuatayo:

Kwanza wanachama tuwe na umoja, tusipende mivutano na mitafaruku ambayo mwisho wake italiathiri tawi letu.

Pili kupenda kutumia taratibu za kidemokrasia katika kufikia maamuzi mbalimbali ndani ya tawi, ili kuweza kujenga na kustawisha uhai wa tawi letu.

Tatu aligusia suala la uchaguzi mkuu wa viongozi wa tawi, hasa ikizingatiwa kuwa idadi kubwa ya wanachama ni wanafunzi. Jambo ambalo linalopelekea kuwa na chaguzi za mara kwa mara kutokana na viongozi kuhitimu masomo na kurejea nyumbani Tanzania. Mwenyekiti alisema kuwa Uongozi wa Tawi uliopo madarakani skwa sasa uko katika hatua za kuandaa uchaguzi huo mapema iwezekanavyo ili Tawi liweze kupata viongozi wengine wapya kwa utaratibu ule ule wa kidemokrasia.

Pia Mwenyekiti alitumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kujitahidi kuendeleza amani na umoja tulivyoachiwa na waasisi wa taifa letu, pia tuondoe tofauti mbalimbali miongoni mwetu ili kujenga jamii yenye uhuru, usawa, haki, upendo, umoja na amani, ambavyo vitapelekea kujenga muonekano na taswira nzuri ya Taifa letu huku ugenini.

Mwisho, Mwenyekiti aliwaomba watanzania wote tuungane kuwaombea wazee wetu waliotangulia mbele za haki, hasa katika wakati huu tunapoomboleza kifo cha Hayati Mzee Nelson Mandela, pia tunapowakumbuka waasisi wa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Hayati Mzee Abeid Amani Karume, Hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa na wengine waliopigania kupatikana kwa Taifa letu.

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA SHEREHE
Mwenyekiti wa Tawi Dkt. Alfred Kamuzora (aliyesimama) akifungua rasmi sherehe hiyo katika ukumbi wa Block 2 uliopo chuoni Lumumba - Moscow. Kutoka kulia, wengine ni: Ndg.Mashango Hassani Mashango (Katibu Mkuu -UVCCM), Bi. Miriam Nungu (Mwenyekiti - UWT), na Ndg.Kassim Kolowa (Katibu Mkuu -Tawi).
Katibu Mkuu wa Tawi Ndg. Kassim Kolowa akiongea wakati wa ufunguzi wa sherehe hiyo.
Mmoja kati ya wanachama wa CCM - Tawi la Moscow akiuliza swali wakati wa sehemu ya mwanzo wa sherehe hiyo, ambapo wanachama walipewa fursa ya kuuliza maswali au kutoa mapendekezo kwa Uongozi wa Tawi.
Mwenyekiti wa Tawi, Dkt. Alfred Kamuzora akijibu maswali ya wanachama.
Katibu wa Siasa na Uenezi , ambaye pia ndiye aliyekuwa mshereheshaji mkuu Ndg. Mbarouk Mahmoud akieleza jambo wakati wa sherehe.
Baadhi ya wanachama wa CCM Tawi la Moscow na watanzania wengine waliohudhuria sherehe hiyo.
Baadhi ya wanachama, watanzania wengine pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria katika sherehe hiyo.
Vijana wakiwa na tabasamu kubwa wakati wa sherehe
Baadhi ya wanachama na watanzania wengine waliohudhuria katika sherehe hiyo.
Mshereheshaji Mkuu Ndg. Mahmoud Mbarouk (kulia, shati jeupe), Mpiga Picha Mkuu Ndg. Omary Nassoro (katikati, shati ya bluu), pamoja na Mtaalamu wa Muziki na Burudani Bw.Cousin Ommy (kushoto, T-shirt Nyekundu) , wakati wa ufunguzi wa sherehe.
Baadhi ya wanachama na watanzania wengine waliohudhuria katika sherehe hiyo.
Mshereheshaji Mkuu Ndg. Mbarouk akitabasamu kushiria mambo yote yanaenda vyema.
Baadhi ya wanachama, watanzania wengine pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria katika sherehe hiyo.
Viongozi wa Tawi , wanachama pamoja na baadhi ya watanzania wakiwa katika picha ya pamoja.
Wakati wa maandalizi kwa ajili ya maakuli wakati wa sherehe.
Wakati wa Maakuli.
Wakati wa Maakuli.
Wakati wa Maakuli.
Mmoja wa wanachama akifurahia jambo na mmoja wa wageni waalikwa.
Katibu Mkuu wa Tawi Ndg. Kolowa pamoja na Mwenyekiti wa UWT Bi. Miriam Nungu 
Baadhi ya Viongozi wa Tawi  pamoja na wanachama wa UWT
Baadhi ya Viongozi wa Tawi  pamoja na wanachama wa UWT
Viongozi wa Tawi, baadhi ya wanachama wa CCM Tawi la Moscow pamoja na baadhi ya watanzania waliohudhuria katika sherehe hiyo, wakiwa katika picha ya pamoja. 

No comments: