CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Wednesday, December 11, 2013

SHEREHE YA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA TANGANYIKA

UONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) TAWI LA MOSCOW - URUSI UNAPENDA KUWAALIKA WATANZANIA WOTE WANAOISHI KATIKA MJI WA MOSCOW NA VIUNGA VYAKE PAMOJA NA MIJI MINGINE KATIKA KUSHEREHEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA TANGANYIKA (09 DESEMBA).

SHEREHE HIYO ITAFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 14.12.2013, KUANZIA SAA KUMI NA MBILI JIONI HADI SAA TATU USIKU , CHUONI LUMUMBA, KATIKA UKUMBI WA HOSTEL No 2 (ULITSA MIKLUHO - MAKLAYA, HOUSE 5, BLOCK 2).
 MGENI RASMI KATIKA SHEREHE HIYO ATAKUWA NI Mhe. JULIUS MJEMA

WEWE MTANZANIA POPOTE PALE ULIPO HUU NI WAKATI WAKO ADHIMU KUKUTANA NA WATANZANIA WENZAKO KATIKA KUSHEREHEKEA SIKU HII IKIWA PIA NI KATIKA KUWAENZI NA KUWATHAMINI MASHUJAA WETU WALIOTETEA TAIFA LETU HADI KUPATA UHURU WAKE.

HIVYO BASI NI WAJIBU WA KILA MTANZANIA NDANI YA MOSCOW NA MIJI MINGINE NCHINI URUSI KUUNGANA PAMOJA KATIKA KUSHEREHEKEA PAMOJA NA MAJIRANI ZETU WOTE PAMOJA NA WAGENI WAALIKWA KWA PAMOJA.

TUFIKE KWA WINGI NA KWA KUZINGATIA MUDA HUSIKA.

WOTE MNAKARIBISHWA  

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA KATIBU WA SIASA NA UENEZI - TAWI ,
Ndg MBAROUK MAHMOUD

No comments: