CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Thursday, December 5, 2013

PONGEZI KWA Dkt. ASHA - ROSE MIGIRO TOKA TAWI LA CCM - MOSCOW

Dkt. Asha-Rose Migiro
Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi tawi la MOSCOW nchini URUSI unapenda kutoa pongezi za dhati kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya Chama cha Mapinduzi Dkt. Asha-Rose Migiro kwa kuteuliwa kuwa mbunge wa heshima.

Uteuzi huo ambao umefanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa mamlaka aliyo nayo kwa mujibu wa Katiba, umeanza rasmi Desemba 3, 2013,

Aidha uongozi wa tawi kwa kupitia mwenyekiti wake Dkt. Alfred Kamuzora umesema kuwa uteuzi huu ni ishara ya wazi kuwa rais Kikwete na chama kwa ujumla umeridhishwa na utendaji pamoja na uwajibikaji wa Dkt. Asha Rose Migiro katika kulitumikia taifa la Tanzania na ni wazi kuwa bado anahitajika zaidi katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya taifa letu.

Mbali na hayo tawi la CCM – Moscow linampongeza na kumuunga mkono Mhe. Rais Kikwete katika jitihada zake za kuthamini kwa dhati nafasi ya mwanamke katika dunia ya sasa. Hiyo pia ni changamoto kwa wanawake wote wa Tanzania katika uwajibikaji na kulitumikia taifa kwa ujumla.

Tawi la CCM - Moscow linamtakia kila la heri na mafanikio zaidi Dkt. Asha-Rose Migiro katika utendaji na uwajibikaji zaidi katika kulitumikia Taifa letu.

IMETOLEWA NA UONGOZI WA TAWI LA CCM MOSCOW-URUSI

No comments: