CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Friday, December 6, 2013

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA RAIS WA AFRIKA KUSINI KUFUATIA KIFO CHA RAIS MSTAAFU NELSON MANDELA

Hayati mzee Nelson Mandela enzi za uhai wake
Julai 18, 1918 - Desemba 05, 2013

Tawi la Chama Cha Mapinduzi Moscow – Urusi , kwa huzuni kubwa linatoa salamu za pole kwa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo mwenye asili ya kiafrika Mzee NELSON MANDELA kilichotokea tarehe 05.12.2013.

Kifo cha shujaa huyo wa Afrika Kusini na bara la Afrika kwa ujumla  ni pengo kubwa sana kutokana na namna ambavyo alivyokuwa na mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya bara la Afrika pamoja na kudumisha Amani na demokrasia nchini Afrika Kusini na  barani Afrika.

Mzee MANDELA atakumbukwa sana na taifa la Tanzania hasa katika ushirikiano wake katika utatuzi wa migogoro mbalimbali ndani ya bara la AFRIKA ambapo aliweza kushirkiana vizuri na aliyekuwa rais wa kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania, Hayati Mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE.

Hayati  baba wa taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa na Hayati mzee Nelson Mandela enzi za uhai wao, katika moja ya mikutano ya Umoja wa nchi za Afrika (OAU)
Watanzania na waafrika wote kwa ujumla yatupasa kumuenzi Hayati Mzee Mandela kwa kulinda na kudumisha Amani, upendo na demokrasia aliyoipigania kwa faida ya bara la Afrika.

TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AMPUMZISHE KWA AMANI SHUJAA WETU MZEE NELSON MANDELA .

No comments: