Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiinua bango kuashiria kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika |
Wanachama wa Chama Chama Mapinduzi tawi la
MOSCOW nchini URUSI kwa kushirikiana na viongozi wao kwa pamoja wanapenda kutumia
fursa hii adhimu kutoa salamu za pongezi kwa watanzania wote popote pale walipo
duniani katika sherehe za maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika (Tanzania
bara kwa sasa) uliopatikana tarehe 09.12.1961.
Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere |
Akitoa
salamu hizo mwenyekiti wa tawi hilo Dkt. Alfred Kamuzora alisema hii ni fursa
nyingine ya watanzania kuungana kwa pamoja katika kuadhimisha siku hii ambayo
ilipiganiwa ili kulipatia uhuru taifa letu.
Aidha
aliongeza kuwa watanzania inabidi kuenzi matunda ya uhuru tulioupata hasa kwa
kuzingatia njia ambayo ilitumika kupata uhuru ambayo haikuwa ya umwagaji damu
hivyo ni wajibu wetu kuilinda amani ambayo waasisi wetu waliipigania kwa hali
na mali ikiwa ni ishara ya kuthamini juhudi zao.
Hayati Meja Alexander Nyirenda akipandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro usiku ule wa mkesha wa siku ya Uhuru wa Tanganyika |
Dkt. Kamuzora alisema kuwa miaka 52 ya uhuru
bila mapigano ni jambo la kujivunia sana hivyo ni wajibu wa kila mtanzania
kuilinda na kuitetea nchi yake popote pale dunia na kuzidi kuiletea sifa
nchi yetu ambayo inasifika kwa Amani na
upendo dunia.
Akimalizia kutoa salamu
hizo Dkt. Kamuzora pia alisisitiza watanzania tuzidi kuliombea taifa letu liwe na amani zaidi.
IMETOLEWA NA UONGOZI WA CCM TAWI LA MOSCOW - URUSI
No comments:
Post a Comment