CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Saturday, February 15, 2014

JK AONGOZA KIKAO MAALUM CHA NEC YA CCM MJINI DODOMA

Mwenyekiti wa CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiongoza kikao cha NEC, leo mjini Dodoma.
Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahiman Kinana na Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) , Dkt. Ali Mohamed Shein.
Mwenyekiti wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete, tarehe 15 Februari, 2014 ameongoza kikao maalum cha NEC, mjini Dodoma.

Katika kikao hicho, Rais Kikwete  amewapongeza viongozi na wanachama wa CCM kwa ushindi uliopatkana katika uchaguzi mdogo wa madiwani ambapo CCM kilishinda katika kata 23 huku CHADEMA kikiambulia kata 3 na NCCR-Mageuzi kikiambulia kata 1. Pia Rais Kikwete alipongeza CCM kwa ushindi ilioupata katika uchaguzi mdogo wa uwakilishi katika jimbo la Kiembesamaki - Zanzibar.

Katika hatua nyingine Rais Kikwete amewataka wana-CCM kuacha kujifanya wanyonge dhidi ya vitendo vya fujo ambavyo vimekuwa vikifanywa na Chadema nyakati za uchaguzi, hasa ikizingatiwa kuwa bado kunatarajia kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa nafasi ya ubunge katika jimbo la kalenga mwezi ujao. Rais Kikwete alisema kuwa ...

"Uchaguzi wa Kalenga ndiyo huo upo mbele yetu, hadi sasa hakuna tatizo lililojitokeza kama Arumeru mambo yapo shwari kabisa, lakini tujue tu kwamba pale tunaenda kushindana na watu (Chadema) ambao wao silaha yao ya kwanza ni fujo... ninaagiza sasa lazima wana CCM kukabiliana na fujo hizo. Unyonge basi. " pia aliongeza ...

CCM kuendelea kujifanya wanyonge kila mara sasa basi. Haiwezekani watu wanafanya fujo hadi wanatoboa watu macho ninyi mnanyongea tu, hili haliwezekani. Tazama pale Igunga mtu wentu alimwagiwa tindikali hadi leo ana ulemavu wa kudumu kisa uchaguzi tu, aah haiwezekani kabisa" alisema Rais Kikwete.

Akiongelea uchaguzi mdogo wa madiwani uliopita, Rais Kikwete alisema kuwa viti vinne kwenda kwa upinzani bado ni doa , hivyo lazima CCM kihakikishe kinazikomboa kata hizo katika chaguzi zijazo.

"Ni kweli tumezoa kata nyingi, lakini kwa kuwa lengo letu CCM kila wakati ni kushinda tu, hatua hiyo ya kuzikosa kata nne bado ni doa lazima kuzikomboa kata hizo chaguzi zijazo ", alisema Rais Kikwete.

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI:
Mwenyekiti wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma.

Mwenyekiti wa CCM , Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali wa CCM mkoa wa Dodoma mara baada ya kuwasili mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa CCM , Dkt. Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM mkoa wa Dodoma wakiangalia ngoma ya jadi wakati wa mapokezi katika uwanja wa ndege wa Dodoma

Mwenyekiti wa CCM , Dkt. Jakaya Kikwete alipowasili katika ukumbi wa Sekretarieti katika jengo la makao makuu ya CCM, mjini Dodoma , kilipofanyika kikao hicho cha NEC.

Rais Kikwete, Dkt. Shein, na Ndg. Abdulrahman Kinana wakiwa wamesimama kuongoza wajumbe wa kikao kuwakumbuka viongozi waliofatiki hivi karibuni.

Wajumbe wa NEC wakimsikiliza mwenyekiti wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete.

Makamu wa Rais Dkt. Bilal (kulia), Waziri Mkuu Mhe. Pinda, pamoja na wajumbe wengine wa NEC, wakiwa ukumbini wakati wa kikao.

Wajumbe mbalimbali wa NEC wakiwa ukumbini wakati wa Kikao.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mbunge wa Igunga Mhe. Dalaly Kafumu

Wajumbe mbalimbali wa kikao cha NEC

Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa UVCCM, Ndg. Sixtus Mapunda, Katibu wa NEC - Itikadi na Uenezi, Ndg. Nape Nnauye, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro, Katibu wa NEC - Uchumi na Fedha, Mama Zakia Meghji, na Katibu Mkuu wa jumuiya ya Wazazi Taifa, 

Dkt. Asha-Rose Migiro (kushoto) na Mama Zakia Meghji (kulia)

Ndg. Martin Shigella na Mhe. Benard Membe wakiteta jambo kwa furaha.

Katibu Mkuu mstaafu wa UVCCM, Ndg. Martin Shigella (kushoto) na Katibu Mkuu wa sasa wa UVCCM, Ndg. Sixtus Mapunda wakiwa ukumbini.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Mwigulu Nchemba (kushoto) akiteta jambo na Katibu wa NEC - Siasa na Uenezi, Ndg. Nape Nnauye.

Wajumbe mbalimbali wakiwa ukumbini wakati wa kikao.

Kutoka kushoto ni Spika wa Bunge Mama Anna Makinda, akifuatiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mzee Kificho.

Wanahabari wakiwa ukumbini wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.

Wajumbe wa NEC , Shamsi Vuai Nahodha na Ally Karume wakiteta jambo nje ya ukumbi.

No comments: