CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Saturday, February 15, 2014

TAARIFA KWA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA


TAARIFA KWA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Kufuatia wito wa Serikali kuwa Wajumbe wote wanaombwa kufika Mjini Dodoma kuanzia tarehe 16 Februari, 2014 katika Viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar wanapenda kuwaarifu Wajumbe wote maandalizi yafuatayo :-  

1.0     USAFIRI WA KUFIKA DODOMA
 • Wajumbe wote wanatakiwa kujigharimia wenyewe kufika Dodoma kwa vyombo vya usafiri wa umma. Wajumbe watarejeshewa gharama za usafiri wa kufika Dodoma kutoka maeneo wanayotoka baada ya kuwasilisha stakabadhi za gharama walizotumia kwa usafiri.
2.0     MALAZI
 • Utaratibu wa malazi umeandaliwa. Hoteli zilizoteuliwa kwa malazi kwa Wajumbe kuchagua kadri itakavyowapendeza zimeainishwa. Hoteli hizo ni hizi zifuatazo :-

 • Wajumbe watalipwa posho ya kujikimu na watalazimika kujitegemea kwa gharama za malazi katika hoteli watakazofikia.
3.0    USAJILI
 • Zoezi la Usajili litafanyika kwenye Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma kuanzia Saa Tatu Asubuhi tarehe 16 Februari, 2014 hadi tarehe 17 Februari, 2014.

 • Zoezi hilo litajumuisha Ujazaji wa Fomu ya Usajili, Upigwaji Picha za Vitambulisho na Kukabidhiwa Begi lenye maelezo muhimu na stahiki nyinginezo kama zitakavyoainishwa.

 • Wajumbe wote wanapaswa kufika na nakala halisi ya vitambulisho vyao ili waweze kutambuliwa kwa  usajili.

 • Vitambulisho vitakavyokubalika ni :-
  1. Shahada ya Kupigia Kura;
  2. Kitambulisho cha Taifa;
  3. Kitambulisho cha Zanzibar;
  4. Hati ya Kusafiria;
  5. Leseni ya Kuendeshea gari;
  6. Kitambulisho cha Mwajiri anayetambulika.
 • Iwapo Mjumbe hana kitambulisho chochote kilichoainishwa hapo juu basi anaombwa kuwasiliana na Maofisa waliotajwa katika tangazo hili kuona namna anavyoweza kusaidiwa.
4.0     MKUTANO WA MAELEKEZO YA AWALI
 • Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katibu wa Baraza la Wawakilishi wameandaa Mkutano wa Maelekezo ya awali siku ya Jumatatu tarehe 17 Februari, 2014 kuanzia Saa Kumi Jioni.

 • Wajumbe wote wanapaswa kuhudhuria Mkutano huo bila kukosa ambao utajumuisha utaratibu wa ukaaji, jiografia ya viwanja vya Bunge na huduma za utawala.

5.0     SHUGHULI ZA KIKAO CHA KWANZA
 • Kikao cha Kwanza kitafanyika Siku ya Jumanne, tarehe 18 Februari, 2014 ambacho kitajumuisha Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda atakayesimamia upitishwaji wa Kanuni na Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
6.0    MAWASILIANO
 • Kwa taarifa zaidi, Wajumbe wanaombwa kuwasiliana na:
 • Ofisi ya Bunge Maalum,
  S.L.P 901,
  DODOMA.

  Simu: 026 23 22 696
  Fax:  026 23 23 116

 • Aidha, Wajumbe wanaweza kupata ufafanuzi zaidi kutoka kwa Maafisa wafuatao :-

  1. Ndg. John Joel
   (0754 260 831)
  2. Ndg. Amour Amour
   (0777 855 878)
  3. Ndg. Kitolina Kippa
   (0754 363 237)
  4. Ndg. Saidi Yakubu
   (0762 089 225)
  5. Ndg. Abdu Haji
   (0779 894 847)
  6. Ndg. Mossy Lukuvi
   (0767 401 333)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU WA BUNGE NA KATIBU WA BARAZA LA WAWAKILISHI
15 FEBRUARI, 2014
**************************No comments: