CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Tuesday, February 11, 2014

KAMATI KUU YA CCM CHINI YA UENYEKITI WA Mhe. Rais, Dkt. JAKAYA KIKWETE YAKUTANA LEO TAREHE 11/2/2014, IKULU - DAR ES SALAAM.

PIA YAMPITISHA Ndg. GODFREY WILLIAM MGIMWA KUWA MGOMBEA UBUNGE KATIKA JIMBO LA KALENGA , IRINGA VIJIJINI KWA TIKETI YA CCM

Mwenyekiti wa CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika leo Ikulu, jijini Dar - es - Salaam.

Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika leo Ikulu, jijini Dar - es -Salaam.

Pamoja na agenda nyinginezo , kikao hicho pia kilimpitisha rasmi Ndg. Godfrey William Mgimwa kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.

Ndg. Godfrey William Mgimwa atapeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo mdogo wa ubunge unaotarajiwa kufanyika tarehe 16 Machi 2014, ili kujaza nafasi iliyo wazi kwa sasa kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Kalenga, Mhe. Dkt. William Mgimwa aliyefariki dunia Januari 1, 2014.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye (Kulia), akimtambullisha Ndg. Godfrey William Mgimwa (kushoto), kwa waandishi wa habari , katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM iliyopo katika mtaa wa Lumumba , jijini Dar - es - Salaam.

Katika hatua nyingine, Katibu wa NEC - Itikadi na Uenezi  Ndg. Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM iliyopo katika mtaa wa Lumumba jijini Dar - es -Salaam, alielezea zaidi kuwa kamati ilimpitisha Ndg. Godfrey W. Mgimwa kwa kuwa amekidhi vigezo ikiwa ni pamoja na kuongoza katika kura za maoni jimboni kwake (Jimbo la uchaguzi la Kalenga).

Godfrey W. Mgimwa ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM, Marehemu Dkt. William Mgimwa.

No comments: