CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Tuesday, February 11, 2014

TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE KATIKA JIMBO LA KALENGA , IRINGA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza rasmi ratiba ya uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kalenga lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini kujaza nafasi ya ubunge iliyo wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mhe. William Mgimwa, ambaye alifariki dunia tarehe 1/1/2014 nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu. 

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi,

> Uteuzi wa Wagombea Ubunge utafanyika tarehe 18 Februari 2014.
> Kampeni za Uchaguzi zitaanza tarehe 19 Februari 2014 hadi 15 Machi 2014.
> Siku ya kupiga kura ni Jumapili tarehe 16 Machi 2014.


No comments: