CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Friday, February 7, 2014

MAJINA YA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA YATANGAZWA

Majina ya watanzania waliopendekezwa na hatimaye kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge maalum la Katiba yametangazwa  leo hii na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Florence Turuka mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mawasiliano Ikulu jijini Dar-es-Salaam.

Bunge hilo ambalo litakuwa na wajumbe 640, litakutana kwa muda wa siku 70 (na kuongezewa siku za ziada 20 endapo hakutokuwa na maafikiano katika baadhi ya masuala muhimu yatakayojadiliwa). Bunge hilo litakuwa na jukumu la kujadili Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba , Desemba 30, 2013.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Florence Turuka akitangaza majina ya wajumbe wa Bunge maalum la Katiba mbele ya waandishi wa habari Ikulu, jijini Dar-es-Salaam.

TAARIFA RASMI

        UTANGULIZI
  1. Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.
  2. Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-

    1. Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
    2. Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
    3. Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c)cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.
  3. Makundi hayo ni  kama ifuatavyo:-

    1. Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)
    2. Taasisi za Kidini (20)
    3. Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);
    4. Taasisi za Elimu (20);
    5. Watu wenye Ulemavu (20);
    6. Vyama vya Wafanyakazi (19);
    7. Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
    8. Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
    9. Vyama vya Wakulima (20); na
    10. Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).
  4.  Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe 02/01/2014.
  5. Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  6. Kufuatia mwaliko huo, taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao. Mapendekezo hayo yalijumuisha majina 2,762 kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar mapendekezo hayo yalihusisha watu 874. Hivyo basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636. Lakini, na kinyume na Sheria, watu 118 walijipendekeza wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.
  7. Mchanganuo wa idadi ya watu walipendekezwa katika makundi mbalimbali ni kama ifuatavyo:

    Na. Kundi/Taasisi Taasisi zilizoleta
    mapendekezo
    Idadi ya Watu
    Waliopendekezwa
    Tanzania Bara Zanzibar Tanzania Bara Zanzibar
    1 Taasisi zisizokuwa za Kiserikali 246 98 1,203 444
    2 Taasisi za Kidini 55 17 344 85
    3 Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu 21 14 129 69
    4 Taasisi za Elimu 9 9 84 46
    5 Makundi ya Walemavu 24 6 97 43
    6 Vyama vya Wafanyakazi 20 1 89 13
    7 Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji 8 1 43 4
    8 Vyama vinavyowakilisha Wavuvi 7 3 45 12
    9 Vyama vya Wakulima 22 8 115 44
    10 Makundi yenye Malengo Yanayofanana 142 21 613 114
    Mapendekezo Binafsi - - 118 -
    Jumla 672 178 2,880 874
    Jumla Kuu 850 3,754

    Na. Kundi/Taasisi Idadi ya Wajumbe Wanaotakiwa Idadi ya Walioteuliwa
    Tanzania Bara Zanzibar
    1 Taasisi zisizokuwa za Kiserikali 20 13 7
    2 Taasisi za Kidini 20 13 7
    3 Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu 42 28 14
    4 Taasisi za Elimu 20 13 7
    5 Makundi ya Walemavu 20 13 7
    6 Vyama vya Wafanyakazi 19 13 6
    7 Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji 10 7 3
    8 Vyama vinavyowakilisha Wavuvi 10 7 3
    9 Vyama vya Wakulima 20 13 7
    10 Makundi yenye Malengo Yanayofanana 20 14 6
    Mapendekezo Binafsi - - -
    Jumla 201 134 67


  8.  Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeweka masharti ya kuzingatiwa katika uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba. Masharti hayo ni pamoja na wajumbe wasiopungua theluthi moja wanatakiwa kutoka Zanzibar na theluthi mbili kutoka Tanzania Bara. Kwa sababu hiyo, katika wajumbe 201, wajumbe 67 watatoka Zanzibar na wajumbe 134 watatoka Tanzania Bara. Aidha, mgawanyo wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa nusu. Pamoja na hayo, wajumbe hao wawakilishe sura ya wananchi wa Tanzania kwa ufuasi wa vyama vya siasa, dini, umri, na maeneo wanayotoka. Katika mazingira haya, zoezi la kupata wajumbe 201 halikuwa rahisi hata kidogo. Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa sana ikilinganishwa na nafasi zilizopo.
  9. Kama nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka Tanzania Bara yalikuwa 2,880 wakati nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande wa Zanzibar, majina yaliyopendekezwa yalikuwa 874 ikilinganishwa na idadi ya wajumbe 67 wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa nyongeza ya maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni kwamba ukichukua taasisi zisizo za kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara walipendekezwa watu 1,203, wakati nafasi zilizokuwa zinatakiwa kujazwa ni 13 tu. Kwa upande Zanzibar, taasisi zisizokuwa za kiserikali zilikuwa zimependekeza majina 444 ikilinganishwa na nafasi 7 tu zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi hizi.


    WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
  10. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakishirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201. Kabla ya kutaja orodha ya wajumbe walioteuliwa, napenda kufafanua mambo yafuatayo:

    1. Uteuzi umezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijana, watu wazima na wazee. Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani wenye umri wa kati miaka 22-35, ni wajumbe 35. Wajumbe wenye umri wa kati, yaani miaka 36-64, ni 145; na wajumbe wazee, yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.

    2. Sheria inataka kuwepo na uwiano sawa kwa ajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili limezingatiwa ipasavyo, na katika orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume 101. Kwa vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe wanaume ni 101.

    3. Uwakilishi wa vyama vya siasa ambao unahitaji kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na wajumbe wawili umezingatiwa. Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu 21, jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe wawili wameteuliwa kutoka katika kila chama.

Baada ya maelezo hayo ya utangulizi, ifuatayo ndiyo orodha ya wajumbe 201 wa Bunge Maalum la Katiba waliobahatika kuteuliwa:



No comments: