Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Jakaya Mrisho Kikwete, jana tarehe 06 Februari, 2014 alizungumza na wajumbe wa Baraza la vyama vya siasa katika ukumbi wa mikutano wa Mwl. Nyerere jijini Dar-es-Salaam. Mazungumzo hayo yalihusu mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia maandalizi ya Bunge la Katiba ambalo linatarajiwa kuzinduliwa muda si mrefu ili kujadili Rasimu ya pili ya Katiba.
|
Rais Jakaya Kikwete akiongea jambo kwa furaha wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa katika Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl.Nyerere, Dar-es-Salaam. |
|
Rais Kikwete akigawa Rasimu ya Katiba kwa viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa waliohudhuria mkutano huo. |
|
Rais Kikwete akitoa hotuba yake kwa wajumbe wa Baraza la vyama vya siasa. |
|
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wakati wa mkutano huo. |
|
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wakati wa maombi mwanzoni mwa mkutano huo. |
|
Rais Kikwete akiwa katika picha pamoja na Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nchini. |
|
Rais Kikwete pamoja na viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa wakitoka katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl.Nyerere jijini Dar-es-Salaam. Mbele kushoto ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad, katikati ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, na kulia ni Msajili wa vyama vya siasa nchini Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi. |
MATUKIO KATIKA VIDEO
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nchini wakiwa katika maombi wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa mkutano wa baraza la vyama vya siasa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Nyerere, jijini Dar-es-Salaam.
(Picha zote kwa hisani ya Issa Michuzi)
No comments:
Post a Comment