CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Tuesday, February 11, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MAANDALIZI YA BUNGE LA KATIBA

Taarifa inatolewa kwamba, Mhe. Anne Semamba Makinda, (Mb.), Spika wa Bunge na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Bunge, mwishoni mwa wiki aliongoza ujumbe wa Tume kufanya ukaguzi wa jengo la Bunge na maeneo ya Bunge ambayo yanakusudiwa kutolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Bunge Maalum.

Wajumbe wa Tume ya Utumishi walioambatana na Spika wa Bunge ni Mhe. Job Ndugai, (Mb.), Naibu Spika na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Beatrice Shellukindo, (Mb.), Mjumbe, Mhe. Hamad Rashid Mohamed, (Mb.), Mjumbe, Dr. Maua Abeid Daftari (Mb.), Mjumbe.

Tume ya utumishi wa Bunge imeridhika kuona kuwa maandalizi yamekamilika na imeridhia kutoa maelezo yafuatayo: -

1.0    UKUMBI WA BUNGE
 1. Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utatumika kwa mikutano ya Bunge Maalum. Ukumbi huo baada ya marekebisho una viti 683 ambavyo vina mchanganuo ufuatao: -

 2. 1.1    Kiti cha Mwenyekiti;
 3. 1.2    Viti vinne (4) vya Makatibu Mezani;
 4. 1.3    Viti vya magurudumu viwili (2) (wheelchairs);
 5. 1.4    Viti 24 vya Wajumbe wenye mahitaji maalum;
 6. 1.5    Viti vya Wajumbe wa Kawaida 652.

 7. Aidha, Ukumbi wa Bunge umewekewa mtambo mpya wa kuzungumzia (Digital Congress Network) kwa Wajumbe wote, ambao una uwezo wa kunakili majadiliano (Hansard) na kuwezesha upatikanaji wa matangazo ya televisheni. Mitambo hiyo ina uwezo pia wa kupiga kura kielektroniki (digital voting).

 8. Pia, ukumbi huo umewekewa mifumo mipya ya usalama.

2.0    KUMBI ZA KAMATI
 1. Ofisi ya Bunge imeandaa na kuratibu upatikanaji wa kumbi kwa ajili ya Kamati kama ifuatavyo: -

 2. NA.UKUMBIMAHALI ULIPOIDADI
  YA WAJUMBE
  1.Ukumbi wa SpikaJengo la Utawala60
  2.Ukumbi Na. 1Hazina Ndogo
  80
  3.
  Ukumbi Na. 2Hazina Ndogo
  80
  4.
  Ukumbi Na. 3Hazina Ndogo
  100
  5.
  Ukumbi Na. 4St. Gasper Hotel
  100
 3. 6.
 4. Ukumbi Na. 5St. Gasper Hotel
  100
  7.
  Ukumbi Na. 6St. Gasper Hotel
  100
  8.
  Ukumbi Na. 7St. Gasper Hotel
  400
  9.
  Ukumbi Na. 8Dodoma Hotel
  200
  10.
  Ukumbi Na. 9Dodoma Hotel
  200
  11.
  Ukumbi Na. 10Msekwa Hall
  250

 5. Kumbi hizo za Kamati zitafungwa vifaa maalum vya sauti kwa lengo la kurekodi majadiliano (Hansard) na kupiga kura.
3.0    MAKTABA
 1. Tume imeridhia Maktaba yake itolewe kwa matumizi ya Bunge Maalum.
4.0    MKAHAWA WA INTERNET
 1. Tume imeridhia Mkahawa wa Internet ulioko katika ghorofa ya pili ya Jengo la Utawala ambayo baada ya marekebisho ina kompyuta 50 itolewe kwa matumizi ya Bunge Maalum.
5.0    ENEO LA UCHAPISHAJI WA NYARAKA
 1. Tume ya Utumishi wa Bunge imetoa mitambo ya kuchapisha nyaraka kwa matumizi ya Bunge Maalum.
6.0    MAENEO YA KUEGESHA MAGARI (PARKING)
 1. Kwa kutambua kwamba idadi ya Wajumbe, watumishi na wageni watakaokuwa wakitembelea Bungeni ni kubwa, Ofisi ya Bunge imeandaa maeneo maalum ya maegesho ya magari ambayo yana uwezo wa kuchukua magari 1,000 kwa wakati mmoja ambayo yatawekewa ulinzi mkali na pia huduma za kawaida.
7.0    ZAHANATI
 1. Tume ya Utumishi ya Bunge imeridhia kutolewa kwa Ukumbi wa Viongozi katika Jengo lenye Ukumbi wa Msekwa kwa matumizi ya Zahanati ya Wajumbe na Watumishi wa Bunge Maalum.
8.0    HUDUMA ZA CHAKULA
 1. Ofisi imekarabati maeneo yake ya huduma za chakula na Tume imeridhia kutolewa kwa kantini mbili kama ifuatavyo: -

 2. 8.1    Kantini iliyoko Jengo la Utawala imekarabatiwa na sasa ina uwezo wa kuchukua watu 300 kwa wakati mmoja.

 3. 8.2    Kantini iliyoko chini ya Ukumbi wa Bunge (Basement) ina uwezo wa kuchukua watu 500 ikiwa na chumba kwa wageni mashuhuri (VIP).
9.0    OFISI
 1. Jengo la Utawala limefanyiwa Marekebisho na kutoa Ofisi 30 ambazo zina uwezo wa kuchukua watu 200. Kati ya hizo, Ofisi nne (4) ni kwa matumizi ya Viongozi wa Bunge Maalum, yaani Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na Naibu Katibu.
10.0    JENGO LA HABARI
 1. Jengo la Habari ambalo lina Ofisi tisa (9) na Ukumbi wa Mikutano limetolewa lote kwa matumizi ya Bunge Maalum.
11.0    MAKAZI YA VIONGOZI
 1. Ofisi ya Bunge imeratibu upatikanaji wa makazi ya Viongozi wa Bunge Maalum ambayo watatumia kwa kipindi chote cha uhai wa Bunge hilo.
Taarifa hii inatolewa kuufahamisha umma kuwa maandalizi yote ya Bunge Maalum yamekamilika na kwamba Tume ya Utumishi wa Bunge ambayo ndio yenye mamlaka ya kusimamia mali za Bunge imeridhia kutolewa kwa maeneo na huduma hizo kama ilivyoainishwa.

Imetolewa na: 
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
S. L. P. 9133,
DAR ES SALAAM. 

10 Februari, 2014

No comments: